MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akizungumza na Watumishi na wasimamizi wa Program ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa . |
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akifurahi pamoja na Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamadudi, Mohammed Mchengerwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu wakisoma Chapisho la Hotuba Mbalimbali za Baba wa Taifa Mwl Julius Kambarage Nyerere alipotembelea maktaba ya wapigania ukombozi Kusini mwa Afrika, alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam.
MAKAMU Mwenyekiti wa Chama Chapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana akipata maelezo ya vifaa mbalimbali Vilivyotumika wakati wa Harakati za ukombozi wa Afrika kutoka kwa Mkurugenzi Msaidizi Sehemu ya Urithi wa Utamaduni na Maadili ya Taifa wa Wizara ya Michezo, Sanaa na Utamaduni, Boniface Kadili huku waziri wa wizara hiyo akishuhudia, wakati Kinana alipotembelea Kituo cha historia ya Ukombozi Kusini mwa Afrika, Dar es Salaam
KINANA ATEMBELEA KITUO CHA UKOMBOZI WA AFRIKA
ATAKA WANANCHI KUJUA HISTORIA
MAKAMU Mwenyekiti wa
Chama Cha Mapinduzi (CCM) Tanzania Bara, Kanali Mstaafu Abdulrahman Kinana,
amesema Chama kinaunga mkono juhudi na malengo ya serikali katika kuenzi,
kutunza na kuendeleza historia ya ukombozi wa Afrika.
Aidha, amewaomba
Watanzania kutembelea kituo cha historia ya ukombozi kilichopo Dar es Salaam
kwa ajili ya kujifunza na kujua kazi kubwa iliyofanywa na wapigania uhuru na
wana ukombozi wa Afrika, huku Tanzania kikiwa kitovu cha harakati hizo.
Kinana aliyasema hayo
Leo, alipotembelea ofisi za Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Bara la Afrika,
na kujionea hatua mbalimbali zilizofikiwa katika kuboresha majengo yake na
kutunza kumbukumbu muhimu.
“Ukombozi wa Afrika
walioshiriki ni wengi, nchinyi zilitoa michango kwa namna mbalimbali, lakini
shgughuli zote hizi ziliongozwa na mtu mmoja bingwa wa mikakati anaitwa Mwalimu
Julius Nyerere. katika Ziara hiyo aliambatana na Waziri wa Michezo, Sanaa na
Utamadudi, Mohammed Mchengerwa pamoja na Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bw. Said Yakubu.