Home » » KUTOKA DODOMA BUNGENI LEO - APRILI 13,2022

KUTOKA DODOMA BUNGENI LEO - APRILI 13,2022

Written By CCMdijitali on Wednesday, April 13, 2022 | April 13, 2022

 

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa

KUTOKA DODOMA BUNGENI LEO - 

APRILI 13,2022


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Serikali itahakikisha bei ya bidhaa zinazozalishwa nchini zinakuwa himilivu wakati ikiendelea kufanya tathmini kwa bidhaa zinazoagizwa kutoka nje ya nchi ili kuona namna ya kuleta unafuu.


Pia, Waziri Mkuu amesema Serikali itaendelea kushirikiana na sekta binafsi hususan wazalishaji na wasambazaji wa bidhaa ili kupanga viwango vipya vya kodi vitakavyoleta unafuu kwa mlaji kama vile kupunguza kodi ya baadhi ya bidhaa.

Mheshimiwa Majaliwa ameyasema hayo leo (Jumatano, Aprili 13, 2022) wakati akihitimisha mjadala wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu, taasisi zake na Mfuko wa Bunge kwa mwaka 2022/2023. Bunge limepitisha kwa kauli moja bajeti hiyo.

Ametumia fursa hiyo kuzielekeza kamati za bei za Mikoa na Wilaya zihakikishe zinafuatilia na kujiridhisha na uhalisia wa kupanda kwa bei za bidhaa kwenye maeneo yao.

Kadhalika, Waziri Mkuu ameendelea kukemea vitendo vya baadhi ya wazalishaji na wafanyabiashara wasiokuwa waaminifu kuamua kupanga bei, kufanya mgomo, kukubaliana katika manunuzi na kuzuia uzalishaji, mbinu ambazo wakati mwingine zimekuwa chanzo cha kupanda kwa bei ya bidhaa.

“Wale wote watakaobainika kufanya michezo hiyo, hatutosita kuwachukulia hatua za kisheria,” amesisitiza.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link