Makamu wa Rais Mhe. Dkt Philip Isidor Mpango |
SERIKALI YAPOKEA GAWIO LA SH.
BILIONI 143 KUTOKA AIRTEL
📌 Dodoma
Makamu wa Rais Mhe. Dkt @dr_philip_isdor_mpango
, amezitaka taasisi binafsi ambazo Serikali imewekeza hisa hata kama ni
asilimia moja kuhakikisha zinajiendesha kwa ufanisi na kulipa gawio
stahiki Serikalini.
Mhe. Dkt. Mpango, ametoa agizo hilo wakati
Kampuni ya Mawasiliano ya simu ya Airtel Tanzania Plc ikiikabidhi
Serikali gawio la shilingi bilioni 143 kama mchango wa uwezeshaji na
mauzo ya minara,
Dkt. Mpango amezitaka taasisi zisizotoa gawio
kujitathmini kwa kuwa Serikali iliwekeza ili faida itumike kwa maendeleo
ya wananchi.
"Taasisi ambazo bado zinatoa gawio dogo na zile ambazo bado zinajiendesha kwa faida, lakini hazitoi gawio stahiki zinatakiwa kujitathmini na kuhakikisha zinafanya vizuri na kulipa gawio Serikalini," alisema Dk Mpango.
Dk Mpango alitoa maagizo hayo wakati akipokea hundi ya Sh bilioni 143 iliyotolewa na Airtel Tanzania Plc kwa mwaka wa fedha 2021/2022 ikiwa ni gawio, mchango wa uwezeshaji na mauzo ya minara. Airtel Tanzania inamiliki asilimia 51 ya hisa zote wakati Serikali ni mmiliki kwa asilimia 49.
Kampuni hiyo kubwa ya pili kwa umiliki wa soko la mawasiliano ya simu nchini, imesema kuwa kati ya fedha hizo, Sh bilioni 88 ni gawio, Sh bilioni 12 mchango wa uwezeshaji (Support Services Agreement (SSA) na Sh bilioni 43 ni kutokana na mauzo ya minara ya mawasiliano ya Airtel kwenda kwa Minara Tanzania Limited.
#kaziiendelee