Naibu
Waziri wa Kilimo, Mhe. Anthony Mavunde, leo tarehe 13 April, 2022 akiwa katika kikao cha 32 cha Shirika la Chakula na Kilimo(FAO) upande wa
Afrika kinachoendelea Jijini Malabo,Equatorial Guinea amepata nafasi ya
kufanya kikao na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Chakula na Kilimo
Duniani(FAO) Ndg. Qu Dongyu na kuwasilisha vipaumbele vya Wizara ya
Kilimo katika kuifikia Agenda 10/30 na kutaka kuendelea kuimarisha
ushirikiano na FAO katika kufikia malengo hayo.
Maongezi hayo yalijikita katika mambo yafuatayo;
1.Kukuza
uwezo wa Taasisi ya Utafiti wa Kilimo(TARI) ili kutimiza malengo yake
ya utafiti na uvumbuzi wa mbegu bora na kanuni bora za kilimo ili
kuwawezesha wakulima wetu kulima kwa tija.
2. Uzalishaji mkubwa
wa mbegu bora kupitia Wakala wa Mbegu Tanzania (ASA) na sekta binafsi
kwa lengo la kupunguza utegemezi wa kuagiza mbegu nje ya nchi na badala
yake kuifanya Tanzania mzalishaji mkubwa wa mbegu zinazitosheleza
mahitaji ya nchi na kuuzwa nje ya nchi.
3.Uwekezaji kwenye Kilimo
cha Umwagiliaji ili kuongeza tija na uzalishaji wa mazao ya kilimo kwa
lengo la kupunguza utegemezi wa kilimo cha mvua amabcho kimekuwa
kikiathiriwa sana na mabadiliko ya tabia nchi.
4.Kuimarisha
huduma za ugani kwa kuwezesha mafunzo maalum ya zao moja moja ili
kuongeza umahiri wa maafisa ugani katika kuwahudumia wakulima na
kuwasaidia kulima kwa tija.
5.Mpango wa ushirikishwaji wa Vijana katika kilimo kupitia mfumo wa mashamba makubwa ya pamoja(_Block farms_).