Home » » TARURA, TANROAD WAKUMBUSHWA KUWEKA MAJINA YA BARABARA ILI KURAHISISHA OPERESHENI ANWANI ZA MAKAZI

TARURA, TANROAD WAKUMBUSHWA KUWEKA MAJINA YA BARABARA ILI KURAHISISHA OPERESHENI ANWANI ZA MAKAZI

Written By CCMdijitali on Tuesday, April 12, 2022 | April 12, 2022

 

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikagua miundombinu ya Anwani za Makazi katika Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi mkoani humo.


Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (kushoto) akikagua miundombinu ya Anwani za Makazi katika Mkoa wa Kilimanjaro wakati wa ziara yake ya mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni ya Anwani za Makazi mkoani humo.


TARURA, TANROAD WAKUMBUSHWA 

KUWEKA MAJINA YA BARABARA ILI

 KURAHISISHA OPERESHENI ANWANI ZA

 MAKAZI

Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nauye amezikumbusha taasisi za TANROAD na TARURA kuweka majina ya barabara ili kurahisisha Operesheni ya Anwani za Makazi

Akizungumza wakati wa ziara ya kukagua mwenendo wa utekelezaji wa Operesheni hiyo Mkoani Kilimanjaro, Waziri Nape amesisitiza kuwa iko hatari ya ukiritimba unaoweza kufanywa na baadhi ya watu kwa kujiita majina ya mitaa yote na barabara kwa kigezo cha kuchangia fedha za utekelezaji wa zoezi la uwekeji wa Anwani za Makazi.

Haya ni maelekezo yaliyotolewa na Waziri Mkuu kwamba TANROAD  na TARURA kwasababu barabara zote ni za kwao wahakikishe wanaweka majina ya hizi barabara ili isaidie kasi ya kukamilisha zoezi hili na mie naomba niwakumbushe watekeleze maelekezo kwa kuweka majina ya hizi barabara ili kuzipunguzia mzigo halmashauri na kuongeza kasi ya utekelezaji wa operesheni  Amesema Waziri huyo

Ameongeza kuwa, viongozi na wananchi wanatakiwa kuwa makini katika kuweka majina ya mitaa kwa kuwa kuna wadau wanajitolea, wanachangia fedha zao lakini ni vizuri majina yawe yenye uzalendo na yanayoendana na uhalisia wa nchi yetu yakiwemo majina ya viongozi pamoja na watu mashuhuri.

Katika hatua nyingine, Waziri Nape ameonesha kuridhishwa na kasi ya utekelezaji wa operesheni hiyo katika Mkoa wa Kilimanjaro ambapo utekelezaji wake umefikia asilimia 99.1.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link