Ujumbe wa Serikali
ya Tanzania unaoongozwa na Katibu Mkuu, Ofisi ya Waziri Mkuu – Kazi, Vijana,
Ajira na Watu Wenye Ulemavu, Prof. Jamal Katundu kwa kushirikiana na Naibu
Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Balozi
Fatma Rajab umetembelea Uwanja wa Kimataifa wa Khalifa ulipo Jijini Doha,
Qatar. Uwanja huo pia unajulikana kama Uwanja wa Taifa, ni moja kati ya uwanja
utakaotumika kwenye mashindano ya Kombe la Dunia yatakayoanza mwezi Novemba
2022.