Home » » RUANGWA MARATHON NI MAALUMU KWA AJILI YA KUCHANGIA VIFAA TIBA

RUANGWA MARATHON NI MAALUMU KWA AJILI YA KUCHANGIA VIFAA TIBA

Written By CCMdijitali on Sunday, September 10, 2023 | September 10, 2023

 


 Na Brown Jonas

 

Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Damas Ndumbaro ameshiriki katika mbio za Ruangwa Marathon ambazo ziliongozwa na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Septemba 9, 2023 Mkoani Lindi.

 

Akizungumza baada ya kumalizika kwa Marathon hiyo Waziri Mkuu Mhe. Majaliwa amesema mbio hizo ni maalumu kwa ajili ya kuchangia vifaa tiba katika vituo vya afya Wilaya ya Ruangwa mkoani Lindi ili kusaidia kuokoa Maisha ya wananchi katika mkoa huo na mikoa Jirani.

 

 

Kwa upande wake Waziri Mhe. Dkt. Ndumbaro ametumia fursa hiyo kutoa wito kwa Wabunge wengine kuandaa mbio kama hizo ili kuibua na kukuza vipaji vya mchezo wa riadha katika maeneo yao hatua itakayosaidia kuwa na timu imara ya taifa ya mchezo huo ambayo itakayokuwa na ushindani ndani na nje ya nchi.

 

Mbio hizo zimehudhuriwa na viongozi mbalimbali wa Serikali, Wadau wa Michezo, Wasanii pamoja na wananchi wa mkoa wa Lindi na mikoa Jirani ambapo mbio zilizoshindaniwa ni KM 5, 10 na 21.









 

 

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link