Home » » KIKAO KAZI CHA WATAALAMU WA UZALISHAJI MALI ,KILIMO ,MIFUGO,MALIASILI,MAZINGIRA ,UTALII,NA WANYAMAPORI MKOA WA ARUSHA

KIKAO KAZI CHA WATAALAMU WA UZALISHAJI MALI ,KILIMO ,MIFUGO,MALIASILI,MAZINGIRA ,UTALII,NA WANYAMAPORI MKOA WA ARUSHA

Written By CCMdijitali on Tuesday, October 10, 2023 | October 10, 2023


Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro Mhe. Mw  Raymond Stephen  Mwangwala amesema serikali itaendelea kushirikiana na Sekta binafsi kutekeleza sera kanuni na miongozo ya kuwaletea wananchi.

Mwangwala amesema  hayo leo Oktoba 10 mwaka huu wakati akifungua  kikao kazi cha wataalam na viongozi kutoka sekta za uchumi na uzalishaji mali yani kilimo,mifugo,uvuvi,maliasili,mazingira,utalii,wanyama pori na ushirika kutoka halmashauri zote za Mkoa wa Arusha kilichofanyika wilayani Ngorongoro.

Pia kikao hicho  kilihudhuriwa na wataalam kutoka Taasisi na Mashirika ya Umma, mashirika yasiyo ya kiserikali NGO's.

"Rai yangu kwenu wataalam wa sekta hizi hakikisheni mnaweka mipango kazi ambayo itapima utendaji  kazi wenu katika kutoa huduma bora kwa wananchi kwa kuongeza  ubunifu, uadilifu, uzalendo, ushirikiano  kupunguza uhasama wa kisekta".


 Katibu Tawala Msaidizi uchumi na uzalishaji mali mkoa wa  Arusha Bw.Chikuturo  amesema uongozi wa mkoa wa Arusha uko tayari kutoa ushirikiano kwa wadau ili kuinua utekelezaji wa sera,miongozo na kanuni Kwa lengo la kuongeza tija kwa wananchi katika sekta katika Sekta hizo.

 "Kikao kazi hiki lengo lake ni  kubadilishana uzoefu, kubainisha changamo na kuweka mikakati ya pamoja kati ya sekta za umma na binafsi Ili kutoa huduma bora kwa wananchi".

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya wilaya ya  Ngorongoro Nasoro Shemzigwa amewataka wataalam hao kutafsiri sera na kanuni mbalimbali za kitaifa na kushusha utekelezaji wake katika ngazi ya chini ya jamii .











Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link