Home » » SERIKALI IMEAMUA KWA DHATI KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA NISHATI

SERIKALI IMEAMUA KWA DHATI KUWEKEZA KWENYE MIRADI YA NISHATI

Written By CCMdijitali on Thursday, January 18, 2024 | January 18, 2024

Published from Blogger Prime Android App

📌 Mkandarasi Mradi wa Julius Nyerere (JNHPP) alipwa kwa asilimia 88.7


📌 Mradi wafikia asilimia 95.8


Dodoma


Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati, Mhe. Dkt. Doto Biteko, ameeleza kuwa, Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan imeamua kwa dhati kuwekeza katika miradi ya nishati nchini huku lengo likiwa ni kuhakikisha kuwa upatikanaji umeme nchini unakuwa mkubwa kuliko mahitaji ya nchi.

Amesema hayo tarehe 18 Januari 2024 jijini Dodoma wakati Wizara ya Nishati ilipowasilisha taarifa kuhusu hali ya uzalishaji na usambazaji umeme nchini kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini.

Kikao ambacho kilihudhuriwa na Naibu Waziri wa Nishati, Mhe. Judith Kapinga, Katibu Mkuu, Mhandisi, Felchesmi Mramba, baadhi ya Wakuu wa Taasisi zilizo chini ya Wizara na Watendaji wa Wizara ya Nishati.

“Moja ya vipaumbele vikubwa vya Serikali ni Sekta hii ya Nishati na ndio maana fedha zimekuwa zikitolewa za kutekeleza miradi mbalimbali ya Nishati ikiwemo mradi mkubwa wa umeme wa Julius Nyerere (JNHPP) ambao gharama yake ni shilingi Trilioni 6.5 na mpaka sasa Serikali imeshamlipa mkandarasi shilingi Trilioni 5.7 ambayo ni sawa na asilimia 88.7.” Amesema Dkt.Biteko

Kuhusu usimamizi wa mradi wa JNHPP amesema kuwa,  Serikali iko makini katika usimamizi  wake na kwamba kuna mamlaka mbalimbali zinazosimamia mradi huo ili ukamilike kwa wakati na kwa ufanisi akitolea mfano Timu Maalum ya Wataalam iliyoundwa na Rais, Dkt. Samia Suluhu Hassan ya kusimamia mradi huo ambayo inaongozwa na Profesa Idris Kikula.

Kuhusu hali ya miundombinu ya umeme nchini, Dkt. Biteko amesema kuwa, itaendelea kufanyiwa matengenezo ili iweze kuzalisha, kusafirisha na kusambaza umeme kwa ukamilifu wake, huku juhudi za kujenga miundombinu mingine mipya ikiendelea.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCO, Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga alieleza Kamati kuwa, mradi  wa umeme wa JNHPP kwa sasa umefikia asilimia 95.8 na kwamba mtambo namba Tisa utakaozalisha megawati 235 umeshakamilika na mtambo Namba 8 na namba 7 iko mbioni kukamilika.

Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
Published from Blogger Prime Android App
@tanesco_official_page @wizara_ya_nishati_tanzania 
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link