Home » » WAZIRI MAKAMBA AMUAGA BALOZI WA DENMARK

WAZIRI MAKAMBA AMUAGA BALOZI WA DENMARK

Written By CCMdijitali on Tuesday, July 9, 2024 | July 09, 2024



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akisalimiana na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing – Spandet aliyemaliza muda wake wa kuhudumu hapa nchini katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba amemuaga Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing – Spandet baada ya kumaliza muda wake wa kuhudumu hapa nchini katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

 

Waziri Makamba amempongeza Balozi Mette kwa kazi nzuri aliyoifanya nchini katika kipindi cha uwakili wake, sio tu kwa kukuza na kudumisha uhusiano wa Kidiplomasia kati ya Tanzania na Denmark vilevile kwa mchango wake hadhimu kwenye utekelezaji wa programu na miradi mbalimbali ya kiuchumi na kijamii ambayo imechangia katika ukuaji wa maendeleo nchini. 

 

Aidha Waziri Makamba amempongeza Balozi Mette kwa mchango wake alioutoa katika kutafuta suluhu ya changamoto mbalimbali zinazoikabili dunia ikiwemo kukabiliana na mabadiliko ya TabiaNchi na masuala ya amani na usalama. 

 

Kwa upande wake Balozi Mette ameeleza kuwa licha kuendelea kukua kwa uhusiano wa kidiplomasia bado juhudi zaidi zinahitajika katika kukuza kiwango cha biashara na uwekezaji katika ya Tanzania na Denmark. 


 Aidha, Balozi Mette ameishukuru Serikali ya Tanzania chini ya Uongozi mahiri wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa ushirikiano mzuri alioupata wakati wote akitimza majukumu yake hapa nchini.

 

Natambua kazi nzuri inayoendelea kufanywa na Serikali ya Tanzania katika kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji nchini, licha kumaliza kipindi changu cha kuhudumu kama Balozi, nitaendelea kutoa mchango wangu kwa namna mbalimbali ili kuhakikisha kiwango cha biashara na uwekezaji baina ya Tanzania na Denmark kinaongezeka.
Alieleza Balozi Mette

 

Tanzania na Denmark zimekuwa zikishirikiana katika sekta mbalimbali ikiwemo kilimo, afya, elimu na biashara na uwekezaji. 



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing – Spandet anayemaliza muda wake wa kuhudumu nchini katika katika picha ya pamoja.


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akifafanua jambo wakati wa mazungumzo na Balozi wa Denmark nchini Tanzania Mhe. Mette Norgaard Dissing – Spandet aliyemaliza muda wake wa kuhudumu nchini yaliyofanyika katika ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mhe. January Makamba akimsikiliza Balozi wa Denmark aliyemaliza muda wake wa kuhudumu nchini Mhe. Mette Norgaard Dissing – Spandet walipokuwa katika mazungumzo yaliyofanyika kwenye ofisi ndogo za Wizara jijini Dar es Salaam.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link