Home » » Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar yafunguliwa

Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar yafunguliwa

Written By CCMdijitali on Wednesday, January 7, 2026 | January 07, 2026

Published from Blogger Prime Android App

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar afungua Maonyesho ya 12 ya Kimataifa ya Biashara ya Zanzibar 


Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Hemed Suleiman Abdulla,amefungua rasmi Maonyesho ya Biashara ya Kimataifa ya 62 ya Zanzibar yanayiendelea katika viunga vya maonyesho vya Nyamanzi, Fumba mjini Unguja.

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa maonesho hayo Makamu wa Pili wa Rais Mheshimiwa Abdulla amesisitiza umuhimu wa maonesho hayo kama chombo cha kukuza biashara, kuongeza fursa za uwekezaji na kuinua sekta ya uzalishaji hasa kwa wajasiriamali wa ndani. 

Alieleza kuwa serikali itaendelea kuwa miongoni mwa waungaji mkono wakuu wa biashara ndogo ndogo, za kati na kubwa ili kuhakikisha ukuaji endelevu wa uchumi wa visiwa vya Zanzibar na Pemba.

Mheshimiwa Abdulla ametembelea mabanda mbalimbali yanayoshiriki katika maonesho hayo ikiwa ni pamoja na banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki na Taasisi zake za AICC,APRM na Kituo cha Uhusiano wa Kimataifa cha Dkt .Salim Ahmed Salim.

Katika banda la Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Mheshimiwa Abdullah Abdullah alipokelewa na Kaimu Mkurugenzi wa Afisi ya Mambo ya Nje Zanzibar Bw. Ally Ally na wafanyakazi wa Wizara walioko katika afisi hiyo.

Mheshimiwa Abdulla amewapongeza watumishi wa Wizara na taasisi zake kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya katika kutekeleza majukumu yao.

Naye Mkurugenzi wa Maonyesho hayo amewataka wadau walioshiriki maonesho hayo kutumia fursa hiyo ya kipekee kuuza bidhaa, kutafuta washirika wa kibiashara na kupanua mitandao ya uwekezaji kwa kuwa maonyesho hayo ni jukwaa muhimu la kukuza soko la ndani na nje ya nchi.

Maonesho hayo yanashirikisha zaidi ya taasisi 316 kutoka serikalini, kampuni binafsi na washirika wa kimataifa yatamalizika Januari 16,2026.

Published from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android AppPublished from Blogger Prime Android App
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link