MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
January 26, 2014
UZINDUZI WA KAMPENI ZA UDIWANI WA CCM WAISAMBARATISHA CHADEMA - SOMBETINI
Written By CCMdijitali on Sunday, January 26, 2014 | January 26, 2014
Labels:
ARUSHA
January 22, 2014
RASIMU YA KATIBA KUTANGAZWA KWENYE GAZETI LA SERIKALI
Written By CCMdijitali on Wednesday, January 22, 2014 | January 22, 2014
Kifungu 20 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83, Toleo la
2013 inamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuchapisha kwenye
Gazeti la Serikali Rasimu ya Katiba ndani ya siku thelathini (30) baada ya
kukabidhiwa rasimu hiyo na Tume ya Mabadiliko ya Katiba.
Taarifa iliyotolewa leo na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi Ombeni Sefue
inaeleza kwamba, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa
Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, alikabidhiwa Rasimu ya Katiba tarehe 30 Desemba,
2013, na ataichapisha kwenye Gazeti la Serikali litakalotolewa Ijumaa, tarehe 24
Januari 2014.
Aidha, kifungu 22 (1) (c) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, Sura 83,
Toleo la 2013, kinampa madaraka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
kwa kushauriana na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi,
kuteua wajumbe 201 wa Bunge Maalumu la Katiba kutoka miongoni mwa majina
yanayopendekezwa kwao na makundi yaliyotajwa ndani ya Sheria hiyo.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, anakusudia kukamilisha
uteuzi wa Wajumbe hao baada ya kushauriana na Rais wa Serikali ya Mapinduzi
Zanzibar, mwanzoni mwa wiki ijayo na majina hayo kuchapishwa kwenye Gazeti
la Serikali kama kifungu 22 (3) cha Sheria iliyotajwa inavyomtaka kufanya.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
Dar es Salaam.
22 Januari, 2014
Labels:
KITAIFA
January 22, 2014
ANGELLAH KAIRUKI ATOA MSAADA WA BAISKELI KWA WOTOTO WENYE ULEMAVU WA VIUNGO
Mheshimiwa akifafanua jambo kuhusu umuhimu wa kuwajali watoto wenye ulemavu kwa wazazi (hawapo pichani) waliofika kupokea msaada wa baiskeli kwa ajili ya watoto wao. Aidha, katika maelezo yake Mhe. Kairuki aliwasihi wazazi kutowaficha ndani watoto walemavu, bali wawapeleke shule na kuwapatia huduma zingine za muhimu ambaza wao kama binadamu wanatakiwa kuzipata. Pia aliwaomba wadau wengine wajitokeze kuwasaidia watoto wenye ulemavu kwani ni ndugu zetu na wanastajili kusaidiwa. Mheshimiwa Kairuki alitoa jumla ya baiskeli 35 kwa watoto wenye ulemavu wa Kawe, jijini Dar es Salaam.
Mheshimiwa Kairuki akimkabidhi baiskeli na vifaa mbalimbali mtoto mmojawapo (jina halikufahamika mara moja) ambaye ni mlemavu wa viungo ili imsaidie wakati wa kwenda shuleni na mahali pengine.
Mheshimiwa Kairuki akimsikiliza Bi. Blandina Sembu ambaye ni Mratibu wa Shirikisho la Vyama vya Walemavu Tanzania (SHIVYAWATA) alipokuwa akitoa shukrani zake kwa Mhe. Kairuki baada ya kukabidhiwa baiskeli 35 kwa ajili ya watoto wenye ulemavu wa viungo katika Kata ya Kawe.
Mmojawapo wa wazazi wa Kata ya Kawe akimshukuru Mhe. Kairuki (hayupo pichani) kwa niaba ya wazazi wenzake kwa moyo wake wa utoaji na wa kuwajali watoto wenye ulemavu na kuwapatia baiskeli zitakazowasaidia kufika shuleni na mahali pengine kwa urahisi.
Baadhi ya watoto wenye ulemavu waliofika kupokea baiskeli hizo kama msaada uliotolewa na Mheshimiwa Kairuki katika harakati zake za kuwasaidia watoto wenye ulemavu.
Labels:
KITAIFA
January 22, 2014
MAKAMU WA RAIS AWASILI ZANZIBAR KUZINDUA KAMPENI KIEMBESAMAKI LEO
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja, Borafya Silima alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar utakaofanyika leo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Katibu wa CCM Mkoa wa Mjini Unguja, Alhajj Rajab Kundiya alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo la Kiembesamaki Zanzibar utakaofanyika leo.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Mgombea Uwakilishi Jimbo la KiembeSamaki CCM Mahmoud Thabit Kombo, alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Abeid Amani Karume Zanzibar leo tarehe 22-2014 kwa ajili ya ufunguzi wa kampeni za uchaguzi mdogo utakaofanyika leo.(Picha na OMR)
Labels:
KITAIFA
January 22, 2014
WAZIRI MKUU KUFANYA ZIARA YA KUKAGUA UJENZI WA BOMBA LA GESI KUTOKA MTWARA NA SONGOSONGO HADI DAR
<
Labels:
KITAIFA
January 22, 2014
DKT. BILAL AZINDUA KAMPENI ZA UCHAGUZI MDOGO JIMBO LA KIEMBESAMAKI LEO
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimtambulisha mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi Ilani Katiba na Sera ya CCM mgombea wa Uwakilishi Jimbo la Kiembesamaki CCM Mahamoud Thabit Kombo kwenye uzinduzi wa kampeni za uchaguzi mdogo wa Uwakilishi wa Jimbo hilo uliofanyika leo 22 Januari 2014 katika uwanja wa Tawi la CCM Kiembe samaki.
(Picha na OMR)
Labels:
KITAIFA
January 22, 2014
MKE WA RAIS MAMA SALMA KIKWETE AZINDUA RASMI MPANGO MPYA WA KUZUIA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI KUTOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO KWA MKOA WA DAR
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akisalimiana na watoto waliozaliwa kutoka katika familia zinazoishi na virusi vya ukimwi lakini zimeweza kupata watoto ambao ni salama baada ya kutumia dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Wazazi wa watoto hao walitoa ushuhuda wao wakati wa sherehe ya uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto (PMTCT OPTION B+) kwa mkoa wa Dar es Salaam zilizofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Julius Nyerere tarehe 22.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwasalimia wazazi wa mtoto Debora Andrew (aliyembeba) , mwenye umri wa miezi 9, ambaye hana maambukizi ya VVU kutoka kwa wazazi wake wanaoishi na virusi vya ukimwi ambao hutumia dawa za kuzuia maambukizi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto. Mama Salma alikutana na wanafamilia hao wakati wa uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi kwa Mkoa wa Dar es Salaam uliofanyika kwenye Ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.
Washiriki waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza na kushangilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akizindua rasmi mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, (PMTCT OPTION B+) kwa Mkoa wa Dar es Salaam katika sherehe iliyofanyika katika ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.
Washiriki waliohudhuria sherehe za uzinduzi wa mwongozo mpya wa huduma za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza na kushangilia hotuba ya uzinduzi iliyokuwa ikitolewa na Mke wa Rais Mama Salma Kikwete aliyekuwa Mgeni rasmi kwenye uzinduzi huo uliofanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akiwapungia mkono washiriki waliohudhuria sherehe ya uzinduzi wa huduma mpya za kuzuia maambukizi ya virusi vya ukimwi kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto kwa Mkoa wa Dar es Salaam. Uzinduzi huo ulifanyika kwenye ukumbi wa Mwalimu Nyerere tarehe 22.1.2014.
PICHA NA JOHN LUKUWI.
Labels:
KITAIFA
January 21, 2014
MAMA SALMA KIKWETE AFUNGUA RASMI MKUTANO WA MAJADILIANO YA WADAU KUHUSU KUTOKOMEZA MAAMBUKIZI YA VVU TOKA KWA MAMA KWENDA KWA MTOTO
Written By CCMdijitali on Tuesday, January 21, 2014 | January 21, 2014
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa Taasisi ya Wanawake na Maendeleo, WAMA, Mama Salma Kikwete akipokewa rasmi na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Mheshimiwa Dkt. Seif Rashid, kwenye hoteli ya Serena alikoenda kufungua mkutano wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto tarehe 21.1.2014.
Mke wa Rais Mama Salma Kikwete akifuatana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dkt. Seif Rashid (kulia) na Mheshimiwa Mama Zakhia Meghji, Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya WAMA, (kushoto), wakielekea kwenye chumba cha mkutano.
Mke wa Rais na Mwenyekiti wa WAMA, Mama Salma Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto uliofanyika kwenye hoteli ya Serena tarehe 21.01.2014.
Dr. Khadija Mwamtemi kutoka hospitali ya Taifa Muhimbili, alikuwa ni mmojawapo kati ya washiriki waliochangia mawazo yao mara baada ya mada mbalimbali kutolewa.
Baadhi ya washiriki wa mkutano wa siku moja wa majadiliano ya wadau kuhusu kutokomeza maambukizi ya virusi vya ukimwi toka kwa mama kwenda kwa mtoto wakisikiliza hotuba ya mgeni rasmi Mama Salma Kikwete (hayupo pichani). Mkutano huo ulifanyika katika hoteli ya Serena hapa Dar es Salaam tarehe 21.1.2014. PICHA NA JOHN LUKUWI
Labels:
KITAIFA
.bmp)



.jpg)
.jpg)



