MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
October 30, 2016
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Mashaka Gambo akimkabdihi Mkuu wa Shule ya
Sekondari Engaranaibo Mwl. Petro Sabatho Tsh 500,000 kwa ajili ya kuchangia ujenzi wa bweni la wasichana katika
Shule hiyo wakati wa ziara yake inayoendelea katika Wilaya ya Longido.
Hili ndilo daraja ambalo wananchi wa Kata ya Mundarara wamejitolea fedha na nguvu zao kuhakikisha ujenzi wa daraja unakamilika na kufanya barabara zinazounganisha vijiji vyao kupitika kipindi chote cha mwaka.
ARUSHA - Wananchi wa Mundarara wajitolea ujenzi wa Daraja
Written By CCMdijitali on Sunday, October 30, 2016 | October 30, 2016
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (aliyeko kwenye mtaro) akishiriki ujenzi wa
daraja la chini linalojengwa na wananchi wa Mundarara.
Viongozi
wa Chama na Serikali Mkoa wa Arusha pamoja na wananchi wa kijiji cha Olgira
Kata ya Mundarara wakielekea kwenye eneo la ujenzi wa daraja ambalo linajengwa
kwa nguvu za wananchi.
Hili ndilo daraja ambalo wananchi wa Kata ya Mundarara wamejitolea fedha na nguvu zao kuhakikisha ujenzi wa daraja unakamilika na kufanya barabara zinazounganisha vijiji vyao kupitika kipindi chote cha mwaka.
Mkuu
wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (katikati) akihamasisha wananchi waendelee
kuchangia ujenzi wa daraja la Mundarara ili liweze kukamilika kwa wakati.
Wanawake
wa Jamii ya Kimaasai maarufu kama Siangiki walijitokeza barabarani kumlaki Mkuu
wa Mkoa wa Arusha wakati wa ziara yake wilayani Longido.
Mabinti
wa jamii ya kimaasai maarufu kama Selengeni pia walishirki mapokezi ya Mkuu wa
Mkoa wakati wa ziara ya kazi wilayani Longido.
Nteghenjwa
Hosseah - Longido
Wananchi wa Kijiji cha Orgirah Kilichopo Kata ya Mundarara Tarafa ya Engarenaibor Wilayani Longido wamelazimika kutumia nguvu zao binafsi kujenga daraja la chini kwa ajili lengo la kuunganisha mawasiliano ya barabara kati ya kata hiyo na kata ya Gelai.
Aidha wamelalamikia kero ya maji tangu mwaka 2013 hadi leo hii hakuna maji yanayotoka kwenye mradi mkubwa wa maji unaofadhiliwa na Benki ya Dunia (WB) unaolenga kusaidia vijiji vitano kwenye kata hiyo.
Wakiongea na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Mrisho Gambo ambaye anaendelea na ziara yake kwenye wilaya hiyo jana, Afisa Mtendaji wa kijiji cha Orgirah, Mathayo Laizer alisema mradi huo wa daraja ni muhimu kwao kwani unafungua fursa za kimaendeleo katika kata mbili za Mundarara na Gelai.
Alisema mradi ulianza mwaka jana na walipata michango mbalimbali kutoka Ofisi ya Mkuu wa Wilaya hiyo ambayo ilitoa Sh. 400,000, Ofisi ya Mkurugenzi Sh, 640,000 na wananchi walichanga Sh, milioni 5.3 lakini ili waweze kukamilisha ujenzi wa daraja hilo wanahitaji mifuko ya saruji 135 pamoja na ndono za kuweka kingo pembeni ya daraja hilo zenye thamani ya Sh milioni 2.9
Naye Esther Mathayo alimuomba Rc, Gambo kuwasaidia kutatua kero ya maji katika kata hiyo ambayo ipo kwenye mradi wa benki ya Dunia tangu mwaka 2013 lakini hadi leo wananchi wanatembea umbali mrefu kutafuta maji hayo kwaajili ya matumizi mbalimbali.
Alisema awali mradi huo uliofadhiliwa na benki ya dunia ulilenga kusaidia vijiji vitano na ulijengwa katika kata hiyo zaidi ya miaka minne iliyopita lakini cha ajabu kwenye chanzo cha maji hakukuguswa na baadhi ya miundombinu imeharibika iliyokwisha wekwa awali sehemu mbalimbali na hawajui ni kwanini umekwama.
Baada ya wananchi kutoa kero zao, Rc Gambo aliwapongeza wananchi hao kwa ujenzi wa daraja hilo la chini kwa kutumia nguvu zao wenyewe kwa kuleta maendeleo ikiwemo kufungua njia za mawasiliano kati ya sehemu moja na nyingine.
"Nawapongeza kwa kazi hii mliyojitolea kwaajili ya kutatua changamoto ya usafiri lakini pia natoa rai kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Longido, Juma Mhina kuhakikisha wanatafuta ufumbuzi wa mradi huu wa maji kama ni fedha watenge kwenye bajeti ya halmashauri hiyo ili wananchi wanywe maji "
Pia aliweza kuchangia mifuko ya saruji 30, pamoja na kufanya harambee na kuchangisha zaidi ya Sh, milioni 1 kutoka kwa watumishi wa sekta mbalimbali alioambatana nao ili daraja hilo liweze kukamilika,awali Gambo kwa kushirikiana na Mkuu wa wilaya hiyo, Daniel Chongolo waliingia ndani ya kingo za daraja hilo kwaajili ya kusaidiana na wananchi kuweka mawe kwenye msingi wa daraja pamoja na wananchi wa kijiji hicho.
Mwisho
Labels:
ARUSHA
October 30, 2016
Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakishangilia Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ulipokuwa unawasili katika Kijiji hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Mbele kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo(Mbele Kulia) wakiwasili kwenye Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Esokonoi.
Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi wakimskilizia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (hayupo pichani) alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano wa hadhara.
ARUSHA - Mtendaji wa Kata aswekwa Rumande kwa Matumizi mabaya ya Fedha za Umma
Wananchi
wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya
Ngorongoro wakionyesha zana walizotumia kutengeneza barabara ya Km 24 kwa nguvu zao wakati wa Ziara ya
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Gambo katika Kijiji hicho.
Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi, Kata ya Gilailumba kata ya Kitumbiine, Wilaya ya Ngorongoro wakishangilia Msafara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha ulipokuwa unawasili katika Kijiji hicho.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisho Gambo(Mbele kushoto) pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Longido Mhe. Daniel Chongolo(Mbele Kulia) wakiwasili kwenye Mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Esokonoi.
Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Arusha Mhe. Michael Lekule Laizer akiongea na
wananchi wa Kijiji cha Esokonoi wakati
wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa katika Wilaya hiyo.
Wananchi wa Kijiji cha Esokonoi wakimskilizia Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo (hayupo pichani) alipokua akizungumza nao kwenye Mkutano wa hadhara.
Mwenyekiti
wa CCM Mkoa Mhe. Michael Lekule Laizer(kushoto), Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe.
Mrisho Gambo (Katikati) pamoja na
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Longido wakiwa katika mavazi ya asili ya Kimasaai
waliyovishwa kwa heshima na wananchi wa Esokonoi.
Watoto wa Jamii ya Kimasaai pia walihudhuria Mkutano wakati wa Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha katika Wilaya ya Longido.
Nteghenjwa Hosseah – Longido
Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Londifo, Juma Mhina ameamuru polisi wa Wilaya hiyo kumkamata na kumuweka ndani Mtendaji wa Kata ya Gilai Lumbwa, Paul Lucas baada ya kutuhumiwa kutumia Fedha za umma vibaya zilizochangwa na wananchi wa maeneo hayo kwa ajili ya kuinua Sekta ya Elimu.
Agizo hilo la Mhina lilifanikiwa baada ya mara kwa mara kushindwa kumkamata Paulo baada ya kumkwepa kila alipokuwa akitafutwa na hatimaye mtendaji huyo kujitokeza kwenye Mkutano wa hadhara wa Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe Mrisgo Gambo uliofanyika kwenye Kijiji cha IIchang Sapukin kata ya Gilailumbwa.
Mmoja kati ya wananchi walioshirki Mkutano huo Bi. Anni Mollel alimshukuru Rc Gambo kufika Kijijini hapo na kujionea hali halisi ya ujenzi wa Shule ya Sekondari ambayo wananchi walichanga Fedha zao zaidi ya Tsh Mil 96 ila hazikutumika kama ilivyokusudiwa badala yake viongozi wa Serikali na Wenyeviti wa Kijiji walitumia Fedha hizo kujinufaisha binafsi badala ya kuwasaidia watoto kukaa kwenye mazingira mazuri ili wapate Elimu.
“Yaan bora umekuja Mkuu hawa viongozi wetu huku kijijini ni Miungu watu wanajipangia mambo yao ya kubadilisha matumizi ya Fedha zilizochangwa na wananchi kaka zao yaan ukiwaangalia wao wana maisha mazuri wakati sisi tunateseka sasa lro uondoke nao na tunamuomba Mkurugenzi wa Halmashauri hii Ndg. Mhina kuwaleta watumishi wengine na wale waliohamishwa hapa baada ya kushirki kula hela zetu wakamatwe pia na waseme wamepeleka wapi hela zetu”
Mara baada ya wananchi kusema hayo Gambo alimhoji Mkurugenzi Mhina ni kwa nini hawajachukua hatua za kisheria kuwakamata watuhumiwa ndipo Mhina aliposema mbele ya hadhara hiyo kwamba zoezi hilo lilishindikana awali baada ya Paulo kumkwepa Mkurugenzi huyo mara kwa mara lakini jana alijileta mwenyewe katika mkutano huo na ndipo imekuwa rahisi kwake kumkamata.
Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Mkaguzi wa ndani wa Halmahauri hiyo, Bi. Mwajuma Mndaira kwenye Mkutano huo alidai kuwa alifanya mahojiano na wenyeviti wa vijiji kujua ni kwa nini walikusanya Fedha kwa wananchi bila kutumia stakabadhi za Serikali katika zoezi hilo.
Pia hivi sasa bado wananendelea na uchunguzi wa nyaraka za malalamiko mbalimbali ili kubaini Paulo alihusika na kinanani na kwa nini abadilishe baadhi ya matumizi ya Fedha hizo na kuuza baadhi ya vitu vilivyochangwa bila kuonyesha sababu ya Msingi kwani baadhi ya kampuni za uwindaji wa kitalii ikiwemo Wingert WindroseSafaris na Kampuni ya Kilombero Nothern Safaris zilitoa mifuko ya Saruji 400 kwa ajili ya ujenzi wa shule ya Sekondari hiyo.
Rc Gambo alimuhoji Mtendaji huyo kwanini shule hiyo haijakamilika mpaka leo wakati watoto wa jamii ya kifugaji wana haki ya Kupata Elimu na wazazi wao wanajitoa wa ajili ya watoto wao huku yeye akiendelea kuwarudisha nyuma, Paulo alijitetea kwamba baadhi ya fedha hizo ziliztumika kihalali na fedha zingine alilazimik kubadilisha matumizi yake na kujenga vyumba vya maabara, jiko pamoja na mabweni.
Baada ya utetezi wake kugonga mwamba alijikuta yupo chini ya himaya ya Polisi waliokuwa wakiongoza msafara huo ambapo pia Mkuu wa Wilaya hiyo Chongolo aliahidi wananchi hao kuwa atafuatilia suala la watumishi wengine watakoziba nafasi za wote watakaomatwa na ubadhirifu huu kuletwa haraka iwezekanavyo ili huduma zisizorote na endapo tuhuma hizi zikithibitkka watapelekwa Mahakamani na aliongezwa kuwa atakua karibu nao kuhakikisha kero kama hizo hazijitokezi rena hapo baadae .
Mwisho
Labels:
ARUSHA

















