MIUNDOMBINU YA ELIMU ZANZIBAR SASA YALINGANA NA MAHITAJI YA KARNE YA 21
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dkt. Hussein Ali Mwinyi, amesema Zanzibar imepiga hatua kubwa katika kuimarisha mazin...
Latest Post
July 09, 2025
Tanzania na Shirikisho la Jamhuri ya Ujerumani kupitia Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) zimesaini Mikataba mitatu ya misaada yenye thamani ya Euro milioni 25.68 (sawa na sh. Bilioni 78.58) kwa ajili ya miradi ya Maji na Maliasili.
Mikataba hiyo imesainiwa katika Ofisi Ndogo za Wizara ya Fedha, jijini Dar es Salaam na Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Dkt. Natu El-maamry Mwamba na kwa upande wa Ujerumani imesainiwa na Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller na Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens.
Dkt. Mwamba alisema kuwa mikataba iliyosainiwa ni kwa ajili ya mradi wa programu ya ufadhili wa miradi ya Maji inanayotegemea matokeo (Investment Financing Facility – Output Based Approach (IFF-OBA) kwa kiasi cha Euro milini 10 sawa na shilingi za Tanzania bilioni 30.6.
Mkataba mwingine ni wa fedha za kufanya upembuzi yakinifu kwa ajili ya mradi wa ustahimilivu wa tabia nchi (Climate Resilient Towns project) kwa kiasi cha shilingi za Tanzania bilioni 2.08.
Alisema kuwa mkataba wa tatu ni wa utekelezaji wa mradi wa Uhifadhi wa Maliasili unaojulikana kama Project for Sustainable Development of Protected Areas kwa kiasi cha Euro milioni 15 sawa na shilingi bilioni 45.9.
Amesema lengo la miradi hiyo ni kutoa motisha kwa Mamlaka za Maji hapa Tanzania kukopa kutoka Benki za Kibiashara kwa ajili ya kujenga miundombinu ya maji ili kuboresha huduma na kuongeza mapato.
Alisema kuwa Kupitia Programu ya IFF – OBA, mamlaka zilizokidhi vigezo zinaweza kukopa kutoka Benki za Biashara na kupatiwa ruzuku kutoka kwenye programu ambapo Mamlaka husika zinapokidhi vigezo, zinaweza kupatiwa ruzuku ya asilimia 50 ya gharama za miradi hadi kufikia kiwango kisichozidi Euro milioni Moja.
Pia mikataba hiyo inalenga uhifadhi na uendelezaji wa maeneo ya Hifadhi za Serengeti na Katavi- Mahale kuhakikisha kunakuwa na uhifadhi na manufaa ya kijamii kwa jamii zinazozunguka hifadhi hizo.
Aidha Dkt. Mwamba ameihakikishia Serikali ya Ujerumani kuwa miradi iliyokusudiwa itatekelezwa kikamilifu na pia Tanzania chini ya Uongozi wa Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kuendelea kuimarisha ushirikiano wa kimaendeleo na Ujerumani kwa manufaa ya watu wa pande zote mbili.
Kwa Upande wake Naibu Balozi wa Ujerumani nchini Tanzania, Mhe. Manuel Muller, alisema kuwa utiaji saini wa mikataba hiyo mitatu ambayo ni sehemu ya muendelezo wa ushirikiano wa kifedha kati ya Tanzania na Ujerumani kupitia benki yake ya maendeleo (KfW).
Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens, alisema kuwa Mikataba hiyo, ni ishara ya hatua nyingine mbele katika ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani ambao umekuwa mzuri tangu miaka ya 1960.
Bw. Christoph Tiskens alisema kuwa, mikataba hiyo miwili itagusa sekta muhimu sana kwa maendeleo ya Tanzania, kupitia awamu ya pili ya Mfuko wa Uwekezaji wa Fedha kwa ajili ya Miundombinu ya Maji (Investment Financing Facility) yenye thamani ya Euro milioni 10, ambayo itafungua fursa mpya kwa mamlaka za maji hapa Tanzania kupitia benki za ndani.
Aliongeza kuwa Mkataba wa pili uliouwekwa saini, unaoitwa "Maendeleo Endelevu ya Mfumo wa Ikolojia ya Maeneo ya Hifadhi", utaimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili pamoja na wadau wa hapa nchini, na mkataba huo unalenga kuimarisha uhifadhi wa maliasili amba oni urithi wa kipekee wa Tanzania na pia kuanzisha minyororo ya thamani kwa ajili ya wananchi wanaoishi karibu na maeneo haya ya asili ya maliasili, ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta ajira.

TANZANIA YAPOKEA MSAADA WA Sh. BILIONI 78.6 KUTOKA UJERUMANI
Written By CCMdijitali on Wednesday, July 9, 2025 | July 09, 2025

“Nina furaha kubwa kufanikisha zoezi hili na Ninawatakia wananchi wa Tanzania maendeleo makubwa, hasa katika Maliasili ambayo pia inamaanisha utalii kuna watalii wengi kutoka Ulaya, hasa kutoka Ujerumani, na hiyo inaleta nguvu kubwa ya kiuchumi kwa nchi, jambo ambalo ni muhimu. Naweza kuwahakikishia kuwa Ujerumani itaendelea kuwa mshirika wa kweli wa Tanzania, Tutaendelea kusimama pamoja nanyi” alisema Mhe. Muller
Naye Mkurugenzi wa Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KfW) anaesimamia nchi za Afrika Mashariki na Umoja wa Ulaya, Bw. Christoph Tiskens, alisema kuwa Mikataba hiyo, ni ishara ya hatua nyingine mbele katika ushirikiano kati ya Tanzania na Ujerumani ambao umekuwa mzuri tangu miaka ya 1960.
Bw. Christoph Tiskens alisema kuwa, mikataba hiyo miwili itagusa sekta muhimu sana kwa maendeleo ya Tanzania, kupitia awamu ya pili ya Mfuko wa Uwekezaji wa Fedha kwa ajili ya Miundombinu ya Maji (Investment Financing Facility) yenye thamani ya Euro milioni 10, ambayo itafungua fursa mpya kwa mamlaka za maji hapa Tanzania kupitia benki za ndani.
“Kipengele cha kupitia benki za ndani ni muhimu sana kwa sababu mbinu hii ya ubunifu inasaidia kukuza miradi inayoweza kufadhiliwa (bankable projects) kwa ajili ya mamlaka za maji, hasa katika mazingira ambayo Tanzania inahitaji kiasi kikubwa cha uwekezaji na fedha” alisema Bw. Tiskens.
Aliongeza kuwa Mkataba wa pili uliouwekwa saini, unaoitwa "Maendeleo Endelevu ya Mfumo wa Ikolojia ya Maeneo ya Hifadhi", utaimarisha ushirikiano wa nchi hizo mbili pamoja na wadau wa hapa nchini, na mkataba huo unalenga kuimarisha uhifadhi wa maliasili amba oni urithi wa kipekee wa Tanzania na pia kuanzisha minyororo ya thamani kwa ajili ya wananchi wanaoishi karibu na maeneo haya ya asili ya maliasili, ili kuchochea ukuaji wa uchumi na kuleta ajira.

Labels:
BIASHARA
July 08, 2025
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa ameitaka Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kuongeza usimamizi wa ukusanyaji wa kodi kwa wafanyabiashara ikiwemo wa mataifa ya nje walioamua kuja kufanya shughuli zao nchini.
Amesema kuwa TRA inapaswa kuongeza ufanisi zaidi kwenye kuwasimamia wafanyabiashara wote kuhakikisha wanatambua sheria za ulipaji kodi pamoja na kufanya ukaguzi wa mara kwa mara ili kuhakiki utekelezaji wake.
Ametoa agizo hilo leo (Jumanne Julai 08, 2025) alipofungua kikao kazi cha Viongozi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) katika kituo cha Mikutano cha Arusha (IACC).
“Nendeni mkachunguze hawa wanaokuja kufanya biashara nchini, kama wanaondoka na mapato yetu kwa kutolipa kodi yetu, ni lazima tubane eneo hilo kama ambavyo sisi tunabanwa tunapokwenda kwao, yeyote aliyeamua kuja kufanya biashara Tanzania ni lazima ajue Tanzania ina sheria zake ikiwemo za ulipaji kodi”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ameipongeza TRA kwa kufanikiwa kukusanya Shilingi Trilioni 32.26, sawa na ufanisi wa asilimia 103.9 dhidi ya lengo la kukusanya Shilingi Trilioni 31.05.
“Hii ni hatua ya kihistoria na ya kujivunia kwa kuwa ni mafanikio yanayoakisi dhamira, weledi, na juhudi mlizonazo zinazofanywa na timu ya TRA na uongozi wote katika kuhakikisha mnafikia malengo mliojiwekea”
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ameiagiza Wizara ya Fedha kuendelea kufanya maboresho ya Sera, sheria na kuimarisha mifumo ya kodi ili kufikia wigo wa juu wa ukusanyaji kodi bila kuathiri ustawi wa shughuli za kiuchumi.
“Kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania, ubunifu mliouonesha mkapata mapato makubwa, endeleeni nao, ubunifu huu umeleta mafanikio makubwa, mbinu rafiki na zakitaalamu mnazotumia kukusanya kodi ziendelezwe, sambamba na kuzingatia Sheria, Utawala Bora, Kanuni na utu”
Kwa upande wake, Waziri wa Fedha Dkt. Mwigulu Nchemba amesema kuwa Wizara hiyo pamoja na TRA wamejipanga kuhakikisha Watanzania wanaelewa kuwa Maendeleo ya nchi yanatokana na kodi.
“Wengi wanadhani kuwa fedha za maendeleo zipo Benki Kuu, tunatakiwa kuendelea kuwaelimisha Watanzania kwamba kila kitu cha maendeleo wanachokiona ni fedha zetu, hata fedha za mkopo ni fedha zetu kwa kuwa tutalipa kwa kodi zetu”
Naye Kamishna Mkuu wa TRA Yusuph Mwenda amesema kuwa katika mwaka wa fedha ulioishia juni 30, 2025, wameweza kuwarejeshea walipa kodi zaidi ya Shilingi trilioni 1.2 kiwango kikubwa tangu kuanza kwa Mamlaka hiyo “Serikali imerejesha ili kuwezesha biashara zifanye kazi”
“Na katika mwaka huu wa fedha tumepanga kukusanya shilingi trilioni 36 ikiwa ni mapato ghafi, tunaamini tukiwa pamoja na walipa kodi tunafanikiwa, tunajua hii ni ndoto ambayo viongozi wetu mnatamani tuitimize”.

MAJALIWA AITAKA TRA KUENDELEA KUONGEZA UFANISI UKUSANYAJI KODI
Written By CCMdijitali on Tuesday, July 8, 2025 | July 08, 2025
- Awapongeza kuvuka lengo 2024- 2025.
- TRA yarejesha Shilingi Trilioni 1.2 kwa walipa kodi kiwango kikubwa kuwahi kutokea.

KITAIFA
July 07, 2025
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Mhe. Dkt. Hussein Ali Mwinyi amesisitiza kuwa dhamira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, kwa kushirikiana na Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ni kuhakikisha mazingira wezeshi ya biashara na uwekezaji yanaimarishwa.
Rais Dkt. Mwinyi amesema kuwa Serikali itaendelea kuwa bega kwa bega na sekta binafsi, wajasiriamali na wawekezaji ili kuhakikisha wananchi wanashirikishwa kikamilifu katika maendeleo ya Taifa.
Rais Dkt. Mwinyi ameyasema hayo leo, tarehe 07 Julai 2025, alipofungua rasmi Maonesho ya 49 ya Biashara ya Kimataifa ya Dar es Salaam (Sabasaba) yaliyofanyika katika Uwanja wa Maonesho wa Mwalimu Julius K. Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Aidha, Rais Dkt. Mwinyi amepongeza mafanikio ya TanTrade na Wizara ya Viwanda na Biashara kwa kuendeleza maonesho hayo na kuyaweka katika viwango vya kimataifa. Amebainisha kuwa mwaka huu, maonesho hayo yamevutia zaidi ya washiriki 5,734 kutoka ndani na nje ya nchi, jambo linalodhihirisha nafasi ya Tanzania kama kitovu cha biashara barani Afrika.
Katika hatua nyingine, Rais Dkt. Mwinyi amezitaka Wizara ya Viwanda na Biashara pamoja na TanTrade kuhakikisha kuwa elimu kuhusu Nembo Maalum ya Taifa kwa bidhaa na huduma za Tanzania (MADE IN TANZANIA) inawafikia wazalishaji na wananchi ili kuchochea uzalendo wa kibiashara.
Amesema uzinduzi rasmi wa nembo hiyo unalenga kuongeza thamani na kutambulisha ubora wa bidhaa za nchi katika soko la kimataifa.
Mapema, Rais Dkt. Hussein Ali Mwinyi alitembelea mabanda ya maonesho ya kampuni za biashara na huduma kutoka ndani na nje ya nchi, pamoja na kukutana na wafanyabiashara na wajasiriamali mbalimbali.
Rais Dkt. Mwinyi alikabidhi zawadi kwa kampuni bora yaliyofanya vizuri zaidi katika Maonesho ya Kimataifa ya Sabasaba 2025, pamoja na Wadhamini Wakuu wa maonesho hayo.
Halikadhalika, alipokea tuzo maalum pamoja na ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa juhudi zao katika kuimarisha maonesho hayo pamoja na kukuza mikakati ya biashara na uwekezaji nchini. Sambamba na hilo, Rais Dkt. Mwinyi alizindua rasmi Nembo Maalum ya Taifa kwa bidhaa na huduma za Tanzania, MADE IN TANZANIA.

RAIS MWINYI:MAZINGIRA YA BIASHARA NA UWEKEZAJI KUENDELEA KUIMARISHWA
Written By CCMdijitali on Monday, July 7, 2025 | July 07, 2025

July 04, 2025
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa huduma za fidia kwa wafanyakazi si suala la hiari bali ni haki ya msingi ya mfanyakazi, inayopaswa kulindwa, kuendelezwa na kusimamiwa kwa weledi na uwajibikaji wa hali ya juu.
Amesema kuwa dhamira ya Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan ni kuendelea kuhakikisha kuwa maendeleo ya nchi yanakwenda sambamba na ulinzi wa haki na ustawi wa wafanyakazi wake.
Amesema hayo leo (Ijumaa, Julai 05, 2025) alipomwakilisha Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan katika ufunguzi wa maadhimisho ya miaka kumi ya Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi (WCF), katika kituo cha Mikutano cha Kimataifa cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam.
“Waajiri, wafanyakazi na Serikali tunapaswa kuendelea kushirikiana kwa dhati katika kuhakikisha kuwa kazi inaendelea kwa tija, na wakati huo huo, wafanyakazi wanalindwa dhidi ya madhila yanayotokana na kazi wanazozifanya kila siku.”
Aidha, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa waajiri wote nchini kuhakikisha wanazingatia kikamilifu matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi ikiwa ni pamoja na kujisajili katika Mfuko, kuwasilisha michango kwa wakati, na kutoa taarifa mapema pale wafanyakazi wanapopata madhila yanayotokana na kazi. ” Kutotimiza wajibu huu ni kutotendea haki ustawi wa wafanyakazi na kulemaza ufanisi wa Mfuko.”
Kadhalika, Mheshimiwa Majaliwa amesema kuwa Rais Dkt. Samia wakati wote ametoa miongozo ya kuhakikisha Serikali inaboresha maslahi ya watumishi wa umma, kuboresha mazingira yakufanyia kazi na Utumishi wa umma kuendeshwa kwa kuzingatia misingi ya utawala bora.
Kwa Upande wake Waziri wa Nchi- Ofisi ya Waziri Mkuu (Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu) Ridhiwani Kikwete amesema kuwa katika jitihada za Serikali ya Awamu ya Sita kuendelea kuboresha ustawi wa Wafanyakazi walioumia kazini, Serikali imekwishatangaza kwenye Gazeti la Serikali Ongezeko la malipo ya fidia ya kila mwezi kwa wanufaika wa Mfuko wa WCF kwa kati ya asilimia 3 hadi asilimia 31 kutegemea mnufaika alistahili kulipwa kuanzia lini.
Ameongeza kuwa WCF imeishi falsafa ya 4R ya Rais Samia Suluhu Hassan ambapo utendaji mzuri wa mfuko huo umeleta mageuzi chanya ya kiuchumi kwa wafanyakazi na kuleta maelewano kati ya wafanyakazi na waajiri. “Kwa kiasi kikubwa hii imewajengea ari ya kufanya kazi kwa bidii na kuongeza uzalishaji hasa tunapoendelea kujenga uchumi wa viwanda”.
Kwa Upande wake Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Dkt. John Mduma ameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita chini ya uongozi wa Rais Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan kwa kupunguza kiwango cha uchangiaji kwa waajiri wa sekta binafsi kutoka asilimia moja wakati Mfuko unaanzishwa hadi asilimia sifuri nukta tano (0.5%) hivi sasa. Hiki kilikuwa ni kilio cha waajiri cha muda mrefu
“Tunaipongeza Serikali pia kwa kuwezesha kupunguza kiwango cha riba ya ucheleweshaji wa michango kwa waajiri kutoka asilimia kumi hadi asilimia mbili kwa mwezi. Hatua hii imeongeza imani ya wawekezaji kwa WCF na Serikali kwa ujumla”.
Naye Mwakilishi mkazi wa Kanda ya Afrika Mashariki wa Shirika la Kazi (ILO) Bi. Caroline Mugalla amesema kuwa katika maadhimisho ya miaka 10 ya WCF, jamii inapaswa kukumbuka kuwa kinga ya jamii sio matumizi yasiyo na tija bali ni uwekezaji katika haki, uzalishaji wenye tija unaolifanya Taifa kuwa thabiti. “Tuendelee kujenga Tanzania ambayo kila mfanyakazi anapata huduma stahiki”
Kwa upande wake Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Waajiri Tanzania (ATE) Suzanne Ndomba-Doran amesema kuwa Chama hicho kwa kushirikiana na WCF wamekuwa wakitoa mafunzo na kuhamasisha waajiri kuhusu fidia kwa wafanyakazi.
“Mafunzo haya yameongeza uelewa na kuchangia kupunguza ajali na magonjwa au vifo vinavyotokana nakazi. Tangu mwaka 2016-2024, ATE kwa kushirikiana na WCF tumefanikiwa kutoa mafunzo mara 21 katika Maudhui Kuhusu Sheria ya Fidia kwa Wafanyakaziya mwaka 2008 na kanuni zake, Fidia Mahali pa Kazi, Ajali na Magonjwa.“
Naye, Naibu Katibu Mkuu wa TUCTA Rehema Ludanga ameipongeza WCF kwa kuimarisha matumizi ya mifumo ya teknolojia ya habari na Mawasiliano ambayo imeweza kuongeza ufanisi na kuhudumia wanachama wake.
“Tunaipongeza sana Serikali kwa kuendelea kuipa nguvu WCF sisi TUCTA tunaahi
di kuendelea kushiriana nao ili mafanikio yazidi kwenda mbele na tunaipongeza kwa kufikia miaka 10 ya faida”
Katika hafla hiyo Mheshimiwa Majaliwa alizindua fao la utengamao ambalo litamuwezesha mfanyakazi aliyepata madhara kazini kurejeshwa ofisini na kupatiwa kazi mbadala inayoendana na hali yake.

HUDUMA ZA FIDIA KWA WAFANYAKAZI SI SUALA LA HIARI-MAJALIWA.
Written By CCMdijitali on Friday, July 4, 2025 | July 04, 2025
- Asema Serikali itaendelea kuhakikisha kunakuwa na ulinzi wa haki na ustawi wa wafanyakazi.
- Atoa wito kwa waajiri kuzingatia matakwa ya Sheria ya Fidia kwa Wafanyakazi.
- Aitaka WCF iendelee kushirikiana na wadau katika sekta ya ajira.

July 03, 2025
WAZIRI MKUU, Kassim Majaliwa amesema kuwa Serikali itaendelea kuimarisha mazingira ya ufanyaji biashara za huduma za kifedha ili kuvutia uwekezaji wa ndani na nje kwa kuwa maendeleo endelevu ya taifa hayawezi kufikiwa bila ushiriki thabiti wa sekta binafsi.
Amesema kuwa sekta ya fedha ni kichocheo kikubwa katika ukuaji wa Uchumi na ustawi wa wananchi kwa ujumla na ni moja ya sababu inyowezesha maendeleo ya Taifa kwenda kwa kasi.
Amesema hayo leo Alhamisi (Julai 03, 2025) wakati wa uzinduzi wa Benki ya Maendeleo PLC, kuwa Benki kamili ya kibiashara, kwenye ukumbi wa mikutano wa hotel ya Hyatt Regency jijini Dar es Salaam.
“Endeleeni kuimarisha ushirikiano miongoni mwenu, serikali kwa kutambua umuhimu wa sekta ya fedha katika kuchagiza maendeleo, imeendelea kuhamasisha matumizi ya teknolojia bunifu”.
Katika hatua nyingine, Mheshimiwa Majaliwa ametoa wito kwa taasisi zote za kifedha zikiwemo benki kuongeza juhudi katika kutoa elimu ya kifedha kwa wananchi ili kuwajengea uwezo wa kuelewa, kutumia na kunufaika na huduma za kifedha kwa maendeleo yao binafsi na kwa ustawi wa taifa kwa ujumla.
“Tukifanya haya tutapunguza wizi, upotevu wa fedha kiholela kwa sababu kila mmoja atakuwa anaweza kujua fedha yake ataipataje, ataihifadhi wapi na namna ya kutoa lakini pia wapeni wateja wenu namna ya utunzaji wa fedha”
Pia, Mheshimiwa Majaliwa ameongeza kuwa kwa mujibu wa takwimu za utafiti wa Finscope huduma jumuishi za fedha zimeweza kukua kutoka asilimia 65 mwaka 2017 hadi kufikia asilimia 76 mwaka 2023. “kwa mujibu wa utafiti huo, matumizi ya huduma za benki yameongezeka na kufikia asilimia 22 mwaka 2023 kutoka asilimia 17 mwaka 2017”.
Kadhalika, Mheshimiwa ametoa wito kwa taasisi zote za fedha zijenge mifumo rahisi na rafiki kwa makundi yote ya watumiaji wa huduma za kifedha.
Awali, Akizungumza kwa niaba ya Askofu Mkuu wa Kanisa la KKKT na Mkuu wa Dayosisi ya Mashariki na Pwani Dkt. Alex Malasusa, Muwakilishi wa Askofu Dean Chadiel Lwiza ameishukuru Benki Kuu ya Tanzania (BOT) kwa kuisimamia benki hiyo na kuwa mfano wa benki iliyoanzishwa na wazawa kwa mtaji mdogo hadi kufikia kuwa benki kitaifa. “Tunaiomba benki kuu jicho lenu liwe kali kuliko letu, itazameni hii benki”
Kadhalika, ameongeza kuwa sera nzuri na mazingira mazuri ya uwekezaji katika biashara na usimamizi mzuri za biashara. “Tunaishukuru Serikali ya awamu ya Sita inayoomgizwa na Rais Dkt. Samia kwa kuendelea kuweka mazingira haya mazuri ya ufanyaji biashara”
Naye Mkurugenzi Mtendaji wa Maendeleo Bank PLC Lomnyaki Saitabau amesema kuwa benki hiyo imejiweka katika nafasi bora zaidi ya kuwa benki ya kisasa, shindani na jumuishi kwa Watanzania wote hasa kipindi dunia inapoelekea kwenye zama mpya zenye msukumo wa kiteknolojia, ubunifu, na uwajibikaji wa hali ya juu.
“Kwa kufanya hivyo, tunaunga mkono juhudi za Serikali ya Awamu ya sita inayoongozwa na Dkt. Samia Suluhu Hassani, yenye dhamira ya kuwafikia watanzania wengi zaidi nchi nzima kupitia dira ya taifa ya ujumuishaji wa kifedha (financial inclusion) na kuchochea maendeleo ya kiuchumi kupitia sekta binafsi, tutaendelea kushirikiana na Serikali, katika ujenzi wa Uchumi wa nchi”.
Naye, Naibu Waziri wa Fedha Hamad Hassan Chande ameipongeza benki hiyo kwa hatua kuwa iliyofikiwa na benki hiyo katika utoaji huduma kwa watanzania hasa kwa kutumia fursa zilizowekwa na Serikali “Sisi Wizara ya Fedha tumeendelea kuweka mazingira mazuri na rafiki ya ufanyaji wa shughuli za kifedha, sasa wekeni mkakati wa kuifikisha benki hii maeneo mengi zaidi”.

SERIKALI ITAENDELEA KUIMARISHA MAZINGIRA YA UFANYAJI BIASHARA-MAJALIWA
Written By CCMdijitali on Thursday, July 3, 2025 | July 03, 2025

KITAIFA/ BIASHARA
July 03, 2025
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Mpango amesema Serikali ya Tanzania ipo tayari kufanya kazi kwa karibu na jumuiya ya wafanyabiashara wa Uhispania kwa kuwa Tanzania na Uhispania zinaweza kuunda ushirikiano wa kiuchumi wenye nguvu ili kuimarisha diplomasia ya kiuchumi.
Makamu wa Rais amesema hayo wakati akifungua Jukwaa la Biashara la Tanzania na Wafanyabiashara wa Uhispania lililofanyika Jijini Sevilla nchini Uhispania leo tarehe 02 Julai 2025. Amesema Tanzania bado inaitambua Uhispania kama mshirika muhimu katika sekta za kimkakati kama vile nishati mbadala, miundombinu, teknolojia ya kilimo, utalii, viwanda vya rasilimali za baharini na biashara.
Makamu wa Rais amesema Tanzania inatambua sekta ya binafsi kama mshirika mkuu katika juhudi za maendeleo inayoongoza katika mabadiliko ya kijamii na kiuchumi. Amewakaribisha wawekezaji hao kuwekeza Tanzania katika fursa mbalimbali zilizopo.
Aidha Makamu wa Rais ameongeza kwamba Tanzania ni Taifa lenye utulivu wa kisiasa, eneo la kimkakati la kijiografia, maliasili nyingi, idadi kubwa ya vijana pamoja na uchumi unaokua kwa kasi. Ameeleza utekelezaji wa mageuzi unaofanywa na serikali ili kuboresha mazingira ya uwekezaji kwa kutambua nafasi muhimu ya sekta binafsi katika maendeleo endelevu.
Makamu wa Rais amesema chini ya uongozi wa Rais Dkt.Samia Suluhu Hassan, Serikali imeimarisha mifumo ya sheria, miundombinu ya kisasa na kuweka dhamira thabiti ya uwazi na utawala bora. Ameongeza kwamba kwa sasa Tanzania ni kivutio cha uwekezaji katika Afrika Mashariki na Kusini mwa Afrika huku ikitoa fursa katika sekta muhimu kama vile biashara ya kilimo, utalii, nishati, madini, viwanda, uchumi wa bluu, na miundombinu.
Makamu wa Rais amewakaribisha kuwekeza katika maeneo ya kimkakati ikiwemo teknolojia ya nishati safi ya kupikia ili kukabiliana na uharibifu wa mazingira unaotokana na matumizi ya mkaa na kuni. Amesema eneo lingine la uwekezaji ni uvunaji wa rasilimali za uchumi wa bluu katika Bahari ya Hindi pamoja na Maziwa Makuu.
Ametaja maeneo mengine ni pamoja na uvuvi na usindikaji, uchunguzi wa madini, utalii wa pwani na baharini, usafirishaji pamoja na uwekezaji katika kuendeleza maeneo ya pwani ya Tanzania na visiwa ili kunufaika na rasilimali za uchumi wa bluu na uhifadhi wa mazingira.
Katika Mkutano huo Viongozi wa Sekta ya Uwekezaji wamewasilisha maeneo mbalimbali ya kuwekeza nchini Tanzania pamoja na kuonesha mageuzi mbalimbali yaliyofanyika nchini ili kuboresha mazingira ya biashara na uwekezaji. Pia wameeleza fursa za uwepo wa soko la uhakika wa bidhaa kutokana idadi ya watu, eneo la kijiographia la Tanzania ambalo linahudumia nchi mbalimbali, uboreshaji wa miundombinu ya msingi pamoja na maendeleo makubwa katika sekta ya TEHAMA.
Jumla ya Makampuni 31 yameshiriki katika Mkutano huo ambayo yamejikita katika uwekezaji kwenye sekta mbalimbali ikiwemo chakula na kilimo, ujenzi wa miundombinu, viwanda, sekta maji, sekta ya madini, nishati, TEHAMA, utalii pamoja na sekta ya fedha.
Mkutano huo umehudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Fedha na Mipango Zanzibar Aboud Mwinyi, Balozi wa Tanzania nchini Hispania mwenye Makazi yake nchini Ufaransa Mhe. Ali Mwadini, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Uwekezaji na Maeneo Maalumu ya Kiuchumi Tanzania (TISEZA) Gilead Teri, Meneja wa Uwekezaji wa Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) Omary Omary, Mkurugenzi Mtendaji wa Sekta Binafsi Raphael Maganga, Katibu wa Baraza la Biashara Tanzania Dr. Godwill Wanga pamoja na Kamishna wa Fedha za Nje Wizara ya Fedha Rished Bade.
Imetolewa na
Ofisi ya Makamu wa Rais
02 Julai 2025
Sevilla – Uhispania.

TANZANIA INAITAMBUA UHISPANIA KAMA MSHIRIKA MUHIMU - DKT MPANGO

KIMATAIFA