Home » » TAIFA Stars yarejea nchini kwa kupitia KILIMANJARO

TAIFA Stars yarejea nchini kwa kupitia KILIMANJARO

Written By CCMdijitali on Tuesday, July 30, 2013 | July 30, 2013



Wachezaji wa Stars wakiwa wamepumzika nje ya hotel ya Nyumbani mjini Moshi.
 
Wachezaji wa Stars.


Meneja wa timu ya Taifa Leopord Tasso Mukebezi akitambulisha mashabiki wa Stars kwa wachezaji wa timu hiyo.

Wachezaji wa Stars wakiingia kwenye gari tayari kuelekea uwanja wa ndege KIA kurejea jijini Dar es salaam.


 TIMU ya taifa ya Tanzania Taifa stars imerejea leo jioni nchini ikitokea Uganda ambako ilikuwa na mchezo wa marejeano wa kufuzu kucheza fainali za wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN)

 Kikosi hicho kimerejea majira ya saa 10:00 Jumapili jioni na ndege ya Precision na kutua katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro ambako walipokelewa na viongozi mbalimbali wa chama cha soka mkoa wa Kilimanjaro.

 Msafara wa timu hiyo uliondoka uwanjanai hapo na kuelekea katika hotel ya Nyumbani iliyopo mjini Moshi ambako kulikuwa kumeandaliwa chakula na mapumziko kabla ya kwenda kupanda ndege kurejea jijini Dar es salaam.

 Hata hivyo licha ya kipigo cha bao 3 kwa 1 kutoka kwa timu ya Uganda mashabiki wa soka katika mji wa Moshi walijitokea katika hotel hiyo kusalimiana na wachezaji huku baadhi wakionesha kusikitishwa na matokeo hayo.

 Na Dixon Busagaga,wa Globu ya Jamii Moshi.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link