Naibu waziri wa maji Dk Binilith
Mahenge akikagua miradi ya maji katika wilaya ya Rombo.
Mhandisi wa maji wilaya ya Rombo
Andrew Tesha akitoa maelezo kwa naibu waziri wa maji Dk Binilith Mahenge
alipotembelea miradi ya maji katika wilaya hiyo.
Naibu waziri wa maji Dk Mahenge
akikagua mradi wa maji wa kilichopo eneo la hifadhi ya Mlima Kilimanjaro (KINAPA)
Naibu waziri Dk Mahenge akizungumza
na mhandisi wa maji wilaya ya Rombo Andrew Tesha alipotembelea kisima cha maji
katika kijiji cha Ushiri.
WIZARA ya maji,imeelezea
kutoridhishwa kwake na uendeshaji wa kampuni ya usambazaji maji wilayani Rombo
ya Kiliwater kwamba haijajipanga kibiashara na ingeweza kupata faida kubwa
kuliko hali waliyonayo sasa kama wangekuwa makini.
Naibu waziri wa maji Dk Binillith
Mahenge alitoa kauli hiyo baada ya kupokea taarifa ya kampuni hiyo kuhusu
usambazaji wa huduma za maji na mipango yao katika ununuzi wa mita kwa ajili ya
kuwafungia wateja wao.
“Kwa mipango hii mliyonayo kama
kampuni hii ingekuwa imekabidhiwa mfanyabiashara yeyote makini,angeshindwa
kupata faida?” alihoji huku mwenyekiti wa bodi ya kampuni hiyo, Silayo akikiri
kwamba faida ingepatikana.
Aliitaka kampuni hiyo kujipanga upya
kwani wanayo fursa ya kupata faida kama wakijitahidi kupunguza maji yanayopotea
lakini pia
kuhakikisha wanaondokana na mfumo wa
ulipaji anka kwa ‘Flat rate’ bali wawafungie wateja mita za maji.
“Huu mfumo wenu wa watu wote kulipa
maji kwa viwango sawa unawapotezea mapato, wapo wanaoyatumia kwa ajili
kumwagilia migomba kasha watalipa sh 3,000 kwa mwezi, ninyi mnaona hilo ni
sahihi,badilikeni”alisema.
Katika baarifa yake kwa naibu waziri
meneja wa Kiliwater, Prosper Kessy alisema uzalishaji wanakabiliwa na
uzalishaji mdogo wa maji usiokidhi mahitaji kwani upo upungufu wa mita za ujazo
13,000 sawa na lita 13,000,000 kwa siku.
Alisema pia wanakabiliwa nupungufu wa
mita za ujazo 22,000 sawa na litaza ujazo 22,000,000 wakati wa kiangazi na
hivyo kuongeza tatizo la maji kwa wateja wake.
“Kiwango kikubwa cha asilimia 78 ya
maji yasiyouzwa kutokana na uchakavu wa miundombinu,wazi wa maji,wateja wasio
na mita na wale wenye mita lakini hutumia maji kiholela”alisema. Hata hivyo
alisema kampuni hiyo inahitaji zaidi y ash milioni 600 kwa ajili ya kuwafungia
mita wateja wake kama njia moja wapo ya kuongeza mapato
Habari na Picha Na Dixon Busagaga wa
Globu ya Jamii Moshi.