Home » » Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya CCM chakutana leo Dodoma

Kikao Maalum cha Kamati Kuu ya CCM chakutana leo Dodoma

Written By CCMdijitali on Sunday, August 25, 2013 | August 25, 2013


Mwenyekiti wa CCM, Rais Jakaya Kikwete akiongoza kikao maalum cha Kamati Kuu ya CCM, Makao Makuu ya CCM, mjini Dodoma leo, Agosti 25, 2013. Kikao hicho kilifanyika kwa ajili ya kukutana Mbunge wa Bukoba mjini Khamis Kagasheki, Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera, Constansia Buhiye, Katibu wa CCM mkoa wa Kagera Abedi Mushi, Mwenyekiti na Katibu wa CCM wilaya ya Bukoba mjini na Meya wa Manispaa ya Bukoba Anatory Amani, kuhusu mgogoro wa madiwani wanane wa CCM Manispaa ya Bukoba. Kulia ni Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana.

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Kagera Ndugu Constansia Muhiye na Katibu wa CCM wa mkoa huo,Ndugu Abedi Mushi wakisubiri kuingia ukumbini kukutana na Kamati kuu mjini Dodoma leo.

Mbunge wa Bukoba mjini Mhe Khamis Kagasheki akiwasili Makao Makuu ya CCM mjini Dodoma.

Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi wa CCM, Ndugu Nape Nnauye akimsikiliza kwa makini Mwana-CCM mwenye ulemavu wa miguu, Shija Luhende kutoka Mwanza, ambaye alimkuta kwenye viwanja vya Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma leo, akitafuta msaada wa baiskeli.

Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Ndugu Abdallah Bulembo akizungumza na Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM,  Ndugu Jenista Mhagama, nje ya ukumbi, Makao Mkuu ya CCM mjini Dodoma, leo.Picha na Bashir Nkoromo.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link