Home » » Mangula: CCM toeni jasho msisubiri uchaguzi

Mangula: CCM toeni jasho msisubiri uchaguzi

Written By CCMdijitali on Friday, October 11, 2013 | October 11, 2013



MAKAMU Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) upande wa Bara, Phillip Mangula, amewataka viongozi wa chama hicho kuhakikisha wanafanya ziara za mara kwa mara ili kukiimarisha chama hicho.

“Hiki ndio kipindi cha kutoa jasho jingi na kukijenga chama na si kusubiri kipindi cha uchaguzi, ndio watu waanze kupita kwa wanachama kuanza kukijenga chama,” alisisitiza Mangula.

Alitoa agizo hilo Dar es Salaam jana katika siku ya pili ya ziara yake mkoani Dar es Salaam, ambapo alianza na wilaya za Kinondoni na Ilala.

Akizungumza na wajumbe wa Halmashauri ya CCM ya Wilaya ya Ilala, alisema viongozi wengi wa chama hicho, hawafanyi juhudi za kukutana na wananchi au kufanya ziara za mara kwa mara na hivyo kutoa mianya kwa vyama vya upinzani kupotosha jamii.

Alikemea tatizo la makundi ndani ya chama hicho na kutaka jitihada zifanyike ili yaweze kuvunjwa, kwani yakiachwa yanaweza kuathiri chama hicho katika uchaguzi ujao.

Akitoa taarifa ya chama, Katibu wa CCM Wilaya ya Ilala, Ernest Chale alisema hali ya kisiasa katika wilaya hiyo, inaridhisha, japo utekelezaji katika baadhi ya maeneo bado unasuasua.

Alitaja mambo yanayosababisha changamoto katika utekelezaji katika wilaya hiyo kuwa ni miundombinu ya barabara, upandaji wa ushuru wa uzoaji taka na maji taka.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link