Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akishiriki kupanda Mwani na baadhi ya Wakulima wa zao hilo la Mwani katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja,kulia kwake ni Muwakilishi wa jimbo la Muyuni ni Mh.Jakhu Hashim Ayoub.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akipokelewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mbunge wa jimbo la Muyuni,Mh.Mahadhi Juma Maalim,mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Pete,jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akisalimiana na Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Muungano Mh.Samia Suluhu Hassani na Mbunge wa jimbo la Makunduchi Samia Suluhu,mara baada ya kuwasili katika kijiji cha Pete,jimbo la Makunduchi, Wilaya ya Kusini Unguja,Pichani kati ni Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman.
Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akisalimiana na Mwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akizungumza na Wajumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Wilaya ya Kusini Unguja,mara baada ya kupokea taarifa fupi ya kazi za chama na taarifa ya utekelezaji wa taarifa ya Ilani ya CCM.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana sambamba na Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Mbunge wa jimbo la Muyuni,Mh.Mahadhi Juma Maalim wakishiriki ujenzi wa ofisi ya CCM katika kijiji cha Kitogani,jimbo la Muyui,wilaya ya Kusini Unguja
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akimjulia hali aliyekuwa mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Kusini Unguja,Ndugu Haji Abdallah Mzee,kulia ni Mwenyekiti Mkoa wa Kusini Unguja,Ndugu Ramadhan Abdallah Ali
Baadhi ya Wakulima wa zao la Mwani wakimsikiliza Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana alipozungumza nao katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana akiwa ameongozana na Mwakilishi wa jimbo la Muyuni, Mh.Jakhu Hashim Ayoub wakielekea kwenye mashamba ya zao la Mwani,ambapo pia Ndugu Kinana alishiriki kupanda Mwani na baadhi ya Wakulima wa zao hilo katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja.
Mmoja wa Wakulima wa Zao la Mwani,akitoa maelezo mafupi namna ya zao hilo linavyopandwa na kutunzwa kwa Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Kinana katika kijiji cha Jambiani,jimbo la Muyuni,wilaya ya Kusini Unguja,kulia kwake ni Muwakilishi wa jimbo la Muyuni ni Mh.Jakhu Hashim Ayoub
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na Muwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman alipowasili katika tawi la CCM Kiunga Mtende,jimbo la Makunduchi wilaya ya Kusini Unguja mapema leo mchana kwa ajili ya kukagua na kushiriki ujenzi wa ukumbi wa tawi la ofisi hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM,Ndugu Abdulrahman Kinana akizindua ukumbi wa mkikutano wa Tawi la CCM Kiunga Mtende,jimbo la Makunduchi wilaya ya Kusini Unguja mapema leo mchana,anaeshuhudia ni Muwakilishi wa jimbo la Makunduchi,Mh.Haroun Ali Suleiman