Waziri Mkuu MIZENGO PINDA amesifu jitihada za walimu wa shule ya sekondari USEVYA iliyopo mkoani KATAVI ambazo zimewezesha shule hiyo kushika nafasi ya kwanza kimkoa kwa kufaulisha wanafunzi wa kidato cha sita.
Aidha shule hiyo ilishika nafasi ya thelathini na nane kitaifa katika matokeo ya mtihani wa kidato cha sita uliofanyika mwaka jana.
Waziri Mkuu PINDA amesema hayo mara baada ya kutembelea shule hiyo na kupongeza juhudi za walimu na wanafunzi na pia akawataka walimu hao kutafuta mbinu zaidi ili shule hiyo iweze kufaulisha zaidi.