Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif akiwa
katika picha ya pamoja na washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la
kukabiliana na maafa Zanzibar yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort.
Kushoto ya Balozi Seif ni Mwakilishi wa shirika la Usafricom
Kamanda Philip Knightsheen, Waziri wa Afya Zanzibar Mh. Rashid Seif , Kaimu
Kamanda wa Brigedia Nyuki Zanzibar na Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla
Mwinyi.
Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh;d Aboud Moh’d, Mwakilishi wa shirika la
Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga, Waziri wa Nchio Ofisi ya Rais
Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omara Kheir, na Msadizi Kamishna wa
Polisi Kamanda Hassan Nassir.
Kamanda Philip Knightsheen akitoa salamu
za Shirika lake linalosimamia huduma za Kibinaadamu na Afya la Usafricom kwenye
mafunzo ya siku tano ya zoaezi la kukabiliana na maafa Zanzibar hapo Zanzibar
Beach Resort Mazizini.
Mwakilishi wa shirika la Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga akizungumza katika mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar.
Waziri wa Ncho Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d akimkabidhi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi Ripoti ya Maafa Zanzibar.
Mkurugenzi wa Idara ya Maafa Zanzibar Nd. Ali Juma Hamad wa kwanza kutoka kulia akiwa na baadhi ya watendaji wa Idara hiyo wanaoshiriki mafunzo ya sku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana maafa Zanzibar yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Baadhi ya washiriki wa mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana maafa Zanzibar yanayofanyika Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini.
Mwakilishi wa shirika la Misaada la Marekani Us Aid Bibi Anna Senga akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif nje ya ukumbi wa Zanzibar Beach Resort mara baada ya kufunguliwa rasmi mafunzo ya zoezi hilo.
Nyuma ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais ,Tawala za Mikoa na Idara Maalum Mh. Haji Omara Kheir. Kulia ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d na Mwakilishi wa Shirika linalosimamia huduma za Kibinaadamu na Afya la Usafricom Kamanda Philip Knightsheen.

Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi
ameipongeza Serikali ya Watu wa Marekani kupitia Shirika lake la Misaada ya
Maendeleo la Us aid kwa jitihada zake za kuisaidia Zanzibar katika mipango yake
ya kutafuta mbinu za kuwa tayari kwa kukabilana na maafa wakati wowote
yatapotokezea.
Alisema Zanzibar imekuwa na historia pana ya majanga mbali
mbali yaliyowahi kuikumba na kusababisha maafa makubwa yatayoendelea kukumbukwa
na vizazi vya sasa na vile vijavyo.
Balozi Seif alitoa pongezi hizo wakati akifungua rasmi
mafunzo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na maafa Zanzibar
yanayofanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Zanzibar Beach Resort Mazizini nje
kidogo ya Mji wa Zanzibar.
Alisema Marekani imekuwa mshirika mkubwa katika kusaidia
harakati mbali mbali za maendeleo ya miundo mbinu ya mawasiliano ya Bara bara,
huduma za Afya na ustawi wa Jamii wa Zanzibar jambo ambalo limekuwa likileta
faraja kwa Wananchi walio wengi hapa Nchini.
Balozi Seif alifahamisha kwamba juhudi za Zanzibar katika
kujiweka tayari kukabiliana na maafa yoyote yatakayoweza kutokea zimekuja
kufuatia majanga tofauti yaliyowahi kutokea kama maradhi ya Kolera, ajali za
vyombo vya usafiri wa Baharini na majanga ya moto ambayo yamesababisha vifo vya
watu kadhaa.
“ Zanzibar imeshuhudia maradhi ya kolera karibu miaka 20 iliyopita na kukumbwa na ajali za usafiri wa Baharini miaka michache iliyopita na kulazimika kuchukuwa jitihada za tahadhari katika kukabiliana nayo endapo yatatokezea tena “. Alisema Balozi Seif.
Alifahamisha kwamba Zanzibar ikiwa miongoni mwa Mataifa
machanga Duniani inawajibika kuimarisha Idara yake ya Maafa kwa kushirikiana na
taasisi za ulinzi, Afya na Mawasiliano ili kuona huduma za kukabiliana na maafa
Nchini zinapatikana kwa ubora unaokusudiwa.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar alieleza kuwa ile nia ya
Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kujenga vituo vya mafunzo na uokozi wakati
yanapotokea maafa katika eneo la Nungwi Mkoa wa Kaskazini Unguja na Chake chake
kwa Pemba bado iko pale pale.
Alisema kilichokwamisha utekelezaji wa mpango huo kwa sasa
ni upatikanaji wa vifaa na fedha licha ya juhudi kadha zinazoendelea
kuchukuliwa na Serikali kuu katika kuomba misaada ya kiufundi kwa Taasisi za
Kimataifa zilizobobea katika taaluma hiyo muhimu.
Balozi Seif alieleza kuwa katika kuimarisha huduma za
kukabiliana na maafa Nchini Mswada wa Sheria ya Kuanzisha Sheria ya Kupunguza
na Kukabiliana na Maafa Zanzibar uliwasilishwa na kujadiliwa na Baraza la
Wawakilishi Zanzibar hivi karibu na hatimae kupitishwa katika Mkutano wa 18 wa
Baraza hilo.
Alisema Mswada huo ulikusudiwa kuweka sheria mpya inayoweka
mfumo wa kisheria katika shughuli za kukabiliana na maafa na mambo ambayo
yataondosha mapungufu yanayoonekana katika sheria iliyopo hivi sasa.
Balozi Seif alisisitiza kwamba Sheria hiyo mpya itawiana na
Sera ya Kukabiliana na Maafa ya mwaka 2011 pamoja na Makubaliano na Mikataba ya
Kikanda na Kimataifa inayohusiana na masuala ya kukabiliana na maafa
iliyoridhiwa na nchi yetu.
Mapema Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Nd. Ahmad Kassim alisema lengo la zoezi hili la
kukabiliana na maafa Zanzibar ni kujenga nguvu za pamoja kati ya Taasisi za
Umma, binafsi zikiungwa mkono na washirika wa maendeleo .
Nd. Ahmad alisema kwa vile majanga yanapotokea yanakumba
kila kilichoko mbele yake ushirikiano wa karibu unahitajika kwa pande zote
zinazohusika ili kujiweka tayari kukabiliana na majanga yoyote yanapotokezea.
Wakitoa salamu za Taasisi zao za kimataifa zinazoshiriki
zoezi hilo Mwakilishi wa Shirika linalosimamia huduma za Kibinaadamu na Afya la
Usafricom Kamanda Philip Knightsheen na Mwakilishi wa shirika la Misaada la
Marekani Us Aid Bibi Anna Senga walisema suala la ulinzi wa maisha ya
Mwanadaamu linamuhusu kila mwana jamii.
Walisema licha ya kwamba nguvu kubwa imewekwa kwa vikosi vya
ulinzi na uokozi kukabiliana na maafa yanapotokea, lakini bado jukumu hilo
litaendelea kusimamiwa kwa pamoja na taasisi zote za umma,binafsi kwa
kushirikiana na washirika wa maendeleo.
Wawakilishi wa taasisi hizo za Kimataifa walisema kwamba
Nchi za Malawi, Msumbiji na Senegal zinazokuwa zikikabiliana na mafuriko ya
mara kwa mara zimekuwa zikipata msaada ya kibinaadamu kwa lengo la kuwapa
matumaini wananchi wake wanaokumbwa na kadhia hiyo.
Waliahidi kwamba Taasisi na mashirika ya maendeleo ya
Kimataifa wakiyatolea mfano yale ya Unicef, WHO,Usafricom,CDHAM na mengine ya
kujitolea yataendelea kuunga mkono juhudi za Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
katika kukabiliana na majanga na maafa wakati yanapotokea.
Akimkaribisha mgeni rasmi kufungua zoezi hilo Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Mh. Moh’d Aboud Moh’d alizishukuru
Taasisi inayohudumia masuala ya Kibinaadamu na Afya { USAFRICOM } na ile ya
kujikinga na Majanga ya Kibinaadamu { CDHAM } kupitia Serikali ya Marekani kwa
kukubali kugharamia mafunzo ya zoezi hilo.
Waziri Aboud alisema msaada wa Taasisi hizo utasaidia
kuwawezesha washiriki wa mafunzo hayo kutoka Mataifa mbali mbali rafiki kupata
taaluma pana itayoweza kuwasaidia katika kutekeleza majukumu yao kwenye taasisi
wanazotokea.
Mafunzo hayo ya siku tano kuhusu zoezi la kukabiliana na
maafa Zanzibar yanayofanyika katika ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Zanzibar
Beach Resort yameshirikisha wawakilishi wa Taasisi za ulinzi, maafa, Utawala,
pamoja na wataalamu wa Afya kutoka nchi mbali mbali Duniani.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
9/2/2015.