Home » » AWAMU YA PILI YA MASHINE ZA BVR KUPELEKWA MIKOA SABA

AWAMU YA PILI YA MASHINE ZA BVR KUPELEKWA MIKOA SABA

Written By CCMdijitali on Tuesday, April 14, 2015 | April 14, 2015

 Tume ya Taifa ya Uchaguzi Nchini Tanzania itaanza kusambaza mashine za BVR 248 katika mikoa saba nchni Tanzania Kuanzia katikati mwa wiki ijayo.

Mikoa iliyopangwa kuanza kupokea mashine hizi ni mikoa ya Lindi, Mtwara,  Ruvuma, Iringa, Wakati zozi likianza mikoa hiyo nyingine zitakuwa zinapelekwa katika mikoa ya Katavi, Mbeya na Dodoma. Mikoa mimgine ni Singida Tabora Geita na Kigoma.

Mkuu wa kitengo cha Ufundi wa idara ya Daftrari/ICT wa NEC Dr Sisit Cariah, Akizungumza na mwandishi wetu amesema kwamba mpaka sasa wanachi wa mikoa ya Lindi, Mtwara, Ruvumna na Iringa wakae tayari kwani muda wowote watatangaziwa vituo vya kujiandikisha.


 Pamoja na mshine hizo 248 Tume ya taifa ya uchaguzi imewaandaa wataalamu 248 ambao watakuwa na jukumu la kutoa elimu kwa wataalamu wengine 50 kwa kila mmoja nchi nzima kwa ajili ya kuharakisha uandikishaji kwa mfumo wa BVR.

Dr Sisit Ameeleza kwamba wamefanikiwa kufanya maboresho makubwa katika mashine hizi ikiwa ni pamoja na kubadilisha upangaji wa vifaa (settings), mfumo endeshi (Software) na upande wa Vichapishio (printer) ambazo sasa zimetengenezewa Nchini Ufaransa umeboreshwa na nirahisi kusafishwa.


 Mafunzo yaliyoendeshwa hapa Jijini Dar es Salaam yamechukua siku moja na yamezingatia sana upande wa Vichapishio (printer), Visoma alama za vidole (Finger Print Scaner) na Kamera kutambua macho mekundu. Ameongoza kwamba printer za sasa ni rahisi kusafishwa na hata kuweka kifaa kipya baada ya cha zamamni kuharibika vimerahisishwa.

Kuhusu uchukuaji wa alama za vidole, amesema kwamba kwa sasa tatitzo la mashine ya kuchukua alama za vidole wamelifanikisha kwa asilimia mia. Kwani kwa wale ambao hawana alama za vidole mashine zimewekewa mfumo wa alogarithim mpya ambao uatatambua kila aina ya kidole.



Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link