Afisa Mkuu wa Mradi wa Teknolojia ya Kisasa ya mawasiliano ya Baharini wa Kampuni ya { SRT } kutoka Nchini Uingereza Bwana Simon Tucker akielezea umuhimu wa kifaa cha mawasiliano kinachotumika katika vyombo vya usafiri Majini kwenye Mkutano wa pamoja na watendaji wa Sekta ya Baharini hapa Zanzibar.
Wa Pili kutoka Kulia waliokaa ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi, Kulia ya Balozi ni Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mh. Said Mohd Dimwa na wa kwanza kulia ni Bwana Lazaria Moh’d Said.
Press Release:-
“ Mkutano wetu wa hivi karibu kati yetu ZMA wenzetu wa SUMATRA ambapo tulishirikisha watendaji wa taasisi za ulinzi wa majini na na polisi bara na Zanzibar ulilenga katika kutafuta mbinu za kujiweka tayari kukabiliana na changamoto yoyote itayojitokeza katika eneo letu “. Alisema Mkurugenzi Abdi.