Gwiji la Taarab asilia enzi zilee Msanii Khamis Juma akiwa miongoni mwa wabunifu na wasanii maalum wanne mwaka huu akikonga nyoyo za washiriki wa hafla ya ugawaji wa Mirabaha kwa wabunifu na wasanii Zanzibar zilizofanyika katika Ukumbi wa Salama Bwawani Mjini Zanzibar.
Mwenyekiti wa Kamati ya ugawaji Mirabaha ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Rahaleo Mh. Salim Nassor Ali –Jazeera akimkabidhi ngao mchangiaji bora wa kusaidia sherehe hizo Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mh. Mahadhi Juma Maalim.
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliyepo kati kati akimkabidhi ngao Msanii Khamis Juma baada ya kufuzu kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar.
Wa kwanza kulia ni Waziri wa Katiba na Sheria Zanzibar Mheshimiwa Aboubakar Khamis Bakari.
Al - Anisa Mwapombe Hiari tetere wa nyimbo za Taarabu aliyevuma ndani ya mwambao wa Afrika katika miaka ile akifurahia zawadi ya ngao na fedha taslim alizokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif baada ya kuwa miongoni mwa wabunifu na wasanii wanne maalum katika sherehe za ugawaji wa Mirabaha Zanzibar.
Berry Black Kijana wa Muziki wa Kizazi kipya akichekelea na kufurahia zawadi aliyokabidhiwa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kwenye sherehe ya ugawaji wa Mirabaha hapo Salama Bwawani Mjini Zanzibar.