Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen M. Wasira, yuko nchini Poland kwa ziara ya kikazi aliyokaribishwa na Waziri Wa Kilimo wa nchi hiyo Marek Sawicki.
Pamoja na mambo mengine, ziara hii inahusu Ujenzi wa kiwanda cha Matrekta ya Ursus na Ujenzi wa Maghala ya kuhifadhi chakula chini ya NFRA.
Katika ziara hiyo Mhe. Wasira ameambatana na Mkuu wa Hifadhi ya Chakula wa Taifa (NFRA) Charles Walwa, pamoja na Maofisa wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika na SUMA JKT.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen M. Wasira (wa pili kulia) na ujumbe wake wakifanya mazungumzo na Waziri wa Kilimo wa Poland Mhe. Marek Sawicki.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen M. Wasira (kulia) akifanya mazungumzo na menejimenti ya kampuni inayotengeneza matrekta ya Ursus katika ofisi za Ursus mjini Warsaw, Poland.
Wajumbe wa Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika wakiwa na mwakilishi wa kampuni ya Ursus Tanzania, Mama Grazyna Tairo.
Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Mhe. Stephen M. Wasira pamoja wa ujumbe wake walivyowasili Warsaw, Poland tarehe 16 April 2015.