Home » » Matayarisho ya ujio wa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Bwana Philipe Jacinto Nyusi ,Zanzibar.

Matayarisho ya ujio wa Rais wa Jamhuri ya Msumbiji Bwana Philipe Jacinto Nyusi ,Zanzibar.

Written By CCMdijitali on Sunday, May 17, 2015 | May 17, 2015

 Mjumbe wa Kamati ya Mapokezi ya Rais wa Msumbiji Maalim Vuai Khamis kutoka Taasisi ya Elimu akikagua Gwaride la Jeshi la Wananchi wa Tanzania {JWTZ } ikiwa ni maandalizi ya mwisho ya ujio wa Kiongozi huyo wa Jamhuri ya Msumbiji Bwana Philipe Jacinto Nyusi anayetarajiwa kufanya ziara ya siku Moja Zanzibar.
 Kamanda Mkuu wa Brigedia Nyuki Zanzibar Bwigedia Jenerali Cyrill Ivor Mhaiki akibadilishana mawazo na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar ambae pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Sherehe na Maadhimisho ya Kitaifa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliyefika uwanja wa Ndege wa Zanzibar kuangalia matayarisho  ya mwisho ya ujio wa Rais wa Msumbiji hapa Zanzibar.
 Balozi Seif akisisitiza jambo wakati alipokagua matayarisho ya mwisho ya Gwaride la kumpokea   Rais wa Msumbiji atakapowasili Zanzibar mapema wiki ijayo.

Kushoto ya Balozi Seif ni Mkurugenzi wa Idara ya Mambo ya Nje Zanzibar Balozi Silima Kombo, Mshauri wa Rais wa Zanzibar katika masuala ya Kiuchumi na Uhusiano wa Kimataifa Balozi Moh’d Ramia, Kamanda wa Brigedia Nyuki Zanzibar Brigedia Jenerali Cyrill Ivor Mhaiki na Mjumbe wa Kamati ya Sherehe na maadhimisho ya Kitaifa kutoka JWTZ Kanali Shaaban Lissu.

 Balozi Seif akikiendesha Kikao cha Kamati ya Mapokezi ya Ujio wa Rais wa Msumbiji Bwana Philipe Nyusi hapo katika jengo la watu mashuhuri     { VIP } Kongwe katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Zanzibar.
 Rais wa Jamuhuri ya Msumbiji Bwana Philipe Jacinto Nyusi.
 Bwa Philipe Jacinto akiwa katika harakati za kampeni wakati wa uchaguzi Mkuu wa Msumbiji ambapo aliinuka kidedea na kuliongoza Taifa hilo katika kipindi cha miaka mitano ijayo.

                                                    Press Release:-

16/5/2015.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link