Wanawakelive kati ya Wanawake walio jitokeza kuchukua fomu ya kugombea Urais 2015 huyu ndio mmoja wapo, Amina S Ali Mgombea Urais Tanzania 2015 haya ndio aliozungumza ndani ya studio zetu za Wanawakelive
(Wasifu )
MAELEZO BINAFSI:
Jina: Amina Salum Ali
Tarehe ya Kuzaliwa: 24 October 1956
Uraia: Tanzania
Jinsia: M/Mke
Anuani : S.L.P 4726
Zanzibar, Tanzania
Barua pepe: ahadizetuziendanenavitendo2015@gmail.com
ELIMU:
- 1979: University of Delhi (India) – B.A Economics
- 1981: University of Pune (India) (Symbiosis College of Management) -MBA in Marketing ( Masoko )
- 1981: Institute of Management Pune, India – Diploma in Financial Management , Operation Research.
- 1983: University of Helsinki, Finland – Diploma in Trade and Export Marketing
UZOEFU WA KAZI
- 1981 – 1982: Mchumi mwandamizi (Senior Economist) Msaidizi Kamishna wa uchumi wa jumla (Macro Economy ) Tume ya Mipango Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar . Majukumu makubwa ni kumsaidia Kamishna katika kupanga mipango ya kitaifa hasa katika Mipango ya pamoja ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (5 years Joint Plan for Tanzania) Mipango ya jumla ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar.
- 1982 – 1983: Mkurugenzi Biashara za Nje – Wizara ya Biashara ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. kushugulikia masuala ya biashara ya nje Zanzibar ,kutengeneza sera za mauzo nje Zanzibar kufanya tafiti ya bidhaa za ziada za kuuza nje na kutafuta matumizi mapya ya bidhaa za Zanzibar zikiwemo viungo kama karafuu ,nazi na mazao yake kama mbata ,mashudu na mafuta ya nazi. Kuratibu mashirikiano na vyombo vya kimataifa vinavyo shgulikia mambo ya mauzo ya nje kama vyombo vya Umoja wa mataifa kama UNCTAD ,ITC na vyombo vya nchi mbali mbali na halmashauri ya Biashara za Nje (TANTRADE) kwa upande wa SMT.
- 1983-1984: Katibu Bodi ya Biashara Zanzibar (Wizara ya Biashara Zanzibar.) Kushugulikia Tenda za manunuzi ya Serikali kufuatilia mauzo ya bidhaa zote za Serikali zinazouzwa nchi za nje.
- Kufuatilia tafiti za Masoko kwa bidhaa za Zanzibar na kujua hali ya Masoko nchi za nje na kuandaa takwimu za biashara za Zanzibar na nchi za nje zinazotumiwa na Tume ya mipango ya Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
- 1984 – 1985: Mchumi Mwandamizi – Tume ya Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
(i) Kushughulikia fedha za nje na mahusiano baina ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar
na nchi marafiki na mashirika ya kimataifa.
(ii) Msaidizi wa Mshauri wa Uchumi wa Zanzibar kushughulikia sheria ya Uwekezaji ambayo ilikuwa ya mwanzo nchini Mashariki ya Afrika (kabla ya nchi zengine kufuatilia katika miaka ya tisini).
- 1985-1990: Mbunge Bunge la Jamhuri ya Muungano ya Tanzania
- 1985 – 1986: Naibu Waziri wa Fedha – Wizara ya Fedha , Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT).Msaidizi mkuu wa Waziri wa Fedha .kushughulikia masuala ya Uchumi na Mipango , matumizi na mapato ya Taifa pamoja na vyombo vya fedha .
- 1986 – 1989: Waziri wa Nchi , Wizara ya Mambo ya Nje, Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania(SMT) anaesimamia Uhusiano wa Kimataifa na wa Kikanda, na vyombo vya Kimataifa na vya kiuchumi kama Umoja wa Mataifa, Jumuiya ya Afrika (OAU) na Tume ya pamoja Mashirikiano na nchi marafiki. Mwenyekiti katika kipindi chote wa Kamisheni hizo (Joint Commissions) na nchi zote marafiki za Afrika, Bara la Asia kama China, Iran, Urusi, Korea ya Kaskazini, Nchi za Marekani ya kusini kama Guyana, Venezuala, Ulaya ya Mashariki (Bulgaria).
- Mwenyekiti wa Vikao vya Mawaziri vya Kanda ya PTA sasa COMESA mwaka 1987, na Vikao vya Mawaziri wa SADC mwaka 1988.
- Mwenyekiti wa Kikao cha Mawaziri wa Fedha na Uchumi cha UNECA mwaka 1987 Ethiopia na Niger.
- Mwakilishi wa Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye vikao vya G77, Mahusiano ya kiuchumi na nchi za Kusini (South South Cooperation) UNECOSOC, na Mwakilishi kwenye vikao vya nchi za Visiwa.
- 1989 – 1990: Waziri wa Nchi, Wizara ya Fedha Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania (SMT) Kushughulikia Mahusiano ya Kimataifa na Kikanda na pia kuratibu suala la kulipa madeni tunayodaiwa na nchi marafiki walio nje ya utaratibu wa Paris (IMF, WORLD BANK)
- 1990 – 2000: Mbunge bunge la Jamhuri ya Muungano
- 1990 – 2000: Mjumbe wa Baraza la Wawakilishi Zanzibar kuteuliwa na Rais na pia Jimbo la Kwahani Zanzibar.
- 1990 – 2000: Waziri wa Fedha, Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar akiwa na jukumu la kusimamia Uchumi wa Nchi Msimamizi Mkuu wa Sera ya Mapato na matumizi ya SMZ, Sera za Uchumi na Fedha na ukuaji wa Uchumi na vyombo vya Fedha zikiwemo Mabenki na Mashirika ya nayo husiana.
- 2001 – 2005: Mjumbe wa Tume ya Mipango, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar . Majukumu ya kusimamia sera za Uchumi ya Zanzibar na masuala yote ya Serikali yanayohusu Mipango ya nchi
- 2005-2006: Mjumbe Baraza la Wawakilishi – nilijiuzulu baada ya kujiunga na AU.
- 2005 – 2006: Waziri wa Nchi ofisi ya Waziri Kiongozi, Serikali ya Mapinduzi Zanzibar.
- Kushughulikia uratibu wa Serikali, Tume ya Uchaguzi, Baraza la Wawakilishi, Sera ya Uwezeshaji wa wananchi na Mashirika yanayotoa mikopo midogo midogo TASAF, Mkurabita nk.
- Uratibu wa mashirikiano na Serikali ya Muungano (SMT), Masuala ya Maafa, Masuala ya walemavu, Masuala ya HIV-Aids na Tume ya Ukimwi ya Zanzibar na Uratibu wa mambo ya ndani ya Nchi Polisi na Uhamiaji.
- 2006 – Mwakilishi wa Kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) Marekani (United States) akiwa kama ni Muwakilishi wa Mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika.
(i) Mshauri wa Kamisheni Umoja wa Afrika kuhusiana mambo ya Afrika huko Marekani.
(ii) Kufuatilia mambo ya Maendeleo ya Afrika huko Marekani kwa kuwajuilisha kuhusu sera mbali mbali za bara la Afrika zinazoendelea na mpya.
(iii). Kuwashajiisha wawekezaji wa Marekani na pia Diaspora wa jamii ya Kiafrika huko Marekani kuwekeza Afrika.
(iv) Kuimarisha uhusiano baina ya Marekani na vyombo vya Serikali, Mabunge na Taasisi za kijamii za Afrika .
(v) Kusaidia kupatikana kwa Fedha za Maendeleo ya Afrika kwa kuzieleza Sera za Maendeleo za Afrika, na kuwashawishi waziunge mkono.
(vi) Kushirikiana na vyombo vya fedha vya Bretton Woods (World Bank na IMF) kwa Maendeleo ya Afrika.
(viii) Kuleta mashirikiano na vyombo vya Elimu ya juu, Mashirika ya Kimataifa, Mifuko ya Maendeleo, Vyombo vya kujitolea na vya hiari (Universities, Research Institutes, Philanthropic Institute Foundations ie Gates, Clinton etc) Kuifahamisha Marekani mambo ya Maendeleo na taarifa njema za kutia moyo na zenye kuleta Maendeleo kwa jamii ya Afrika kwa wamarekani, kwa kutumia vyombo vya habari vyenye Taarifa sahihi.
(xv) kuratibu shughuli za ofisi za kibalozi za Afrika kwa lengo kubwa la kuweza kuwa na sauti ya pamoja katika masuala muhimu ya Afrika na maendelo yake pia na mahusiano na serikali ya Marekani
UZOEFU KATIKA CHAMA
- 1968: Nilijiunga na Umoja wa Vijana wa ASP (ASP Youth League) na kuendelea na Uanachama hadi kuzaliwa kwa CCM mwaka 1977
- 1977: Nilijiunga na Chama Cha Mapinduzi baada ya kuunganishwa kwa vyama vya ASP na TANU na kuzaliwa CCM
- 1987 – 2006: Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya Chama cha Mapinduzi hadi nilipolazimika kujiuzulu kufuatia kuteuliwa kuwa Mwakilishi wa kudumu wa Umoja wa Afrika (AU) huko Marekani. Mlezi wa Jumuiya ya Vijana Mjini
- 1992 – 2006: Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Mapinduzi hadi nilipojiuzulu kufuatia kujiunga na Umoja wa Afrika (AU)
- 2003 – 2006: Makamo Mwenyekiti wa Jumuiya wa Wanawake ya Chama cha Mapinduzi , nafasi niliyolazimika kujiuzulu baada ya kuteuliwa kuwa mwakilishi wa Umoja wa Afrika Marekani.
- 1987 – 2006: Mjumbe wa Kamati mbalimbali zilizoundwa na Chama kwa kipindi chote nilichokuwa Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama cha Mapinduzi.
- Mlezi wa mkoa Morogoro.
- Mlezi wa umoja wa vijana Zanzibar wilaya ya Mjini.
SHUGHULI ZA KIJAMII
- 1990: Mwanzilishi wa Jumuiya isiyo ya Kiserikali (NGO) ya kwanza kuhamasisha Maendeleo ya Wanawake (Catalyst Organisation for Women Progeress in Zanzibar)
- 1995: Mwanzilishi wa Zanzibar Welfare Trust, na pia nimekuwa mlezi wa Zanzibar NGO Clusters.
- Aidha alikuwa Mwanzilishi wa Umoja wa Wawakilishi Wanawake katika Baraza la Wawakilishi la Zanzibar.
- Mwanzilishi wa mfuko wa Rais wa Kujitegemea
BODI MBALIMBALI
- 1992 – leo Mwenyekiti wa Jumuiya isiyo ya Kiserikali ya kuendeleza Wanawake Zanzibar (Catalist Organisation for Women Progress in Zanzibar) –COWPZ
- 1992-1995: Mjumbe Bodi ya Biashara za nje Wizara ya Biashara na Viwanda SMT.
- 1996 – 1999: Mjumbe wa Bodi ya Shirika la Magazeti ya Chama Uhuru na Mzalendo
- 2002- 2005: Mjumbewa baraza la chuo kikuu Cha mzumbe (Mzumbe university council)
- 2003 – 2004: Mjumbe wa Bodi ya Biashara ya Nje, Wizara ya Biashara na Viwanda – Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania
- 2003 – 2005: Mjumbe wa Mfuko wa Elimu Zanzibar, Wizara ya Elimu Serikali ya Mpinduzi ya Zanzibar.
- 2004 – 2005: Mjumbe wa Bodi maalum iliyoshughulika na kazi za Maendeleo ya Wanawake katika Benki ya Maendeleo ya Kiislamu (JEDDAH)
- 2004 – 2006: Mdhamini wa Jumuiya zisizo za Kiserikali Zanzibar (Zanzibar NGO Clusters – ZANGOC zinazoshughulika na masuala ya Ukimwi (HIV – AIDS)
- LUGHA: Kiswahili na Kiingereza – Kuongea na Kusoma kwa Ufasaha
Mh. Amina Salum alipotembelea Ikulu ya Marekani (White House). Picha ni pamoja na Rais wa Marekani Barak Obama
Mh. Amina Salum Ali akiwa anaongoza Ujumbe wa Tanzania katika mazungumzo ya ushirikiano wa Tume ya Pamoja na Serikali ya China.
MH. Amina Salum Ali akisaini mkataba nchini China.
MH. Amina Salum Ali akiwa mkuu msafara nchini China kushoto ni MH. JK enzi hizo.
Mwaka 1987.
Mikutano ya hadhara ya CCM. Alikua na cheo cha Makamu Mwenyekiti UWT, Mjumbe wa Kamati Kuu CCM na Halmashauri Kuu CCM – Zanzibar
Mh. Amina Salum Ali akiwa ni mwenyeji wa Mama Theresa.
Mh. Amina Salum Ali alipotembelea ofisi ya Secretary of State John Kerry.
Mh. Amina Salum Ali alipochukua fomu za kugombea Urais wa Zanzibar mwaka 2000 – Zanzibar.
Wakati wa kampeni – Jimbo la Kwahani 1995