Home » » Balozi Seif Ali Iddi azindua rasmi matangazo ya mfumo wa ununuzi wa nyumba kwa njia ya fedha taslimu na mkopo

Balozi Seif Ali Iddi azindua rasmi matangazo ya mfumo wa ununuzi wa nyumba kwa njia ya fedha taslimu na mkopo

Written By CCMdijitali on Sunday, August 16, 2015 | August 16, 2015

 Mkurugenzi wa Kampuni ya CPS Live inayotarajiwa kujenga Nyumba za Mkopo katia Eneo Huru la Uwekezaji Fumba Bwana Sebastian Dietzold akimkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alipowasili eneo hilo kuzindua matangazo ya mfumo wa ununuzi wa nyumba hizo.

Nyuma ya Balozi Seif ni Mkuu wa Mkoa Mjini Magharibi Mh. Abdulla Mwinyi na wa kwanza kutoka kushoto ni Mkurugenzi wa Huduma za Vitega Uchumi na Maendeleo wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Ndugu Sharif Ali Sharif.
 Mkurugenzi wa Kampuni ya CPS Live Bwana Sebastian Dietzold akimueleza Balozi Seif taaluma inayotumika katika ujenzi wa Nyumba za Mkopo ambapo asilimia kubwa wanatumia mali ghafi za hapa Zanzibar.


 Baadhi ya sehemu za ndani za Nyumba za mfano zilizojengwa kwenye eneo Huru la Uwekezaji liliopo Fumba Wilaya ya Magharibi “B”.
 Bwana Sebastian akimkaguza Balozi Seif katika baadhi ya nyumba vya nymba za mfano zilizojengwa kwenye eneo hilo loa Fumba.
Bwana Sebastian akimfahamisha Balozi Seif Ali Iddi utaratibu wa kubonyeza kitufe kwenye Kompyuta kuashiria uzinduzi rasmi wa matangazo ya mfumo wa ununuzi wa nyumba za Mkopo zitakazojengwa Fumba Eneo huru la Uwekezaji Uchumi.
Picha na – OMPR – ZNZ.

 Press Release:-

Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi alisema kwamba ujenzi wa Nyumba elfu 1,500 zinazotarajiwa kujengwa katika eneo Huru la uwekezaji Vitega Uchumi katika ukanda wa Fumba utasaidia kupunguza ufinyua wa makaazi kwa Wananchi wazalendo pamoja na wawekezji wanaoamua kuanzisha miradi yao hapa Zanzibar.

Alisema ujenzi huo unaofanywa na Kampuni ya Kimataifa ya CPS Live ya Nchini Ujerumani ambayo tayari imeshasajiliwa hapa Zanzibar utaenda sambamba na kutoa ajira kwa kundi kubwa la Vijana wanaomaliza masomo yao.

Balozi Seif Ali Iddi alitoa kauli hiyo wakati akizindua rasmi matangazo ya mfumo wa ununuzi wa nyumba hizo kwa njia ya fedha taslimu na mkopo uliotayarishwa na Kampuni hiyo hapo katika eneo linalotarajiwa kujengwa nyumba hizo Fumba Wilaya ya Magharibi “B”.

Alisema Wawekezaji wengi pamoja na baadhi ya wananchi watapata fursa ya kuondokana na tabia ya kukodi nyumba jambo ambalo huwapa gharama kubwa kulitekeleza.

Balozi Seif alifahamisha kwamba Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefarajika kuona kwamba Wawekezaji wameanza kuitikia wito wa Serikali wa kuanza kuonyesha ishara ya kuwekeza katika eneo hilo muhimu kwa uchumi wa Taifa.

“ Nyumba hizo kwa mujibu wa nilivyoziona ni nzuri zikiwa katika eneo safi na kiwango kijnachokubalika kimataifa na itategemea mhusika mwenyewe hadhi na thamani ya nyumba atayohitaji kununua au kukopeshwa “. Alisema Balozi Seif.

Aliwaomba Wananchi wenye uwezo na wale wawekezaji wenye miradi ya kudumu hapa Nchini kuunga mkono katika ununuzi au ukopaji wa nyumba hizo ili kuondokana na matatizo ya makazi.

Akimkaguza Balozi Seif kuona sampuli ya nyumba za mfano zilizojengwa kwenye mradi huo Mkurugenzi wa Kampuni ya CPS Live Bwana Sebastian Dietzold alisema ujenzi huo utaanza na Nyumba 416 katika awamu ya kwanza.

Bwana Sebastian alisema sehemu hiyo iliyopimwa kitaalamu kwa kuzingatia mipango miji itagaiwa kwa kujengwa nyumba kumi kwa kila kipande kimoja ambapo suala la mazingira itazingatiwa katika hali inayokubalika.

Alifahamisha kwamba utunzaji wa mazingira ni suala litakalotiliwa mkazo kwa kuandaliwa taratibu maalum wa kutolewa elimu utakaohusisha wanafunzi maskulini.

Bwana Sebastian alieleza kwamba huduma za lazima zitazingatiwa kwa kupatikana kwenye nyumba zote zitakazojengwa eneo hilo sambamba na ujenzi wa Kituo cha Polisi, Hospitali viwanja wa michezo mbali mbali pamoja na maeneo ya mapumziko.

Mapema Mkurugenzi wa Huduma za Vitega Uchumi na Maendeleo wa Mamlaka ya Uwekezaji Vitega Uchumi Zanzibar { ZIPA } Ndugu Sharif Ali Sharif alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ilitangaza kwamba Fumba ni eneo Tengefu la Uwekezaji mwaka 1992.

Nd. Sharif alisema Fumba sasa imefumbuka kutokana na mwanzo mzuri wa uanzishwaji wa miradi ya kiuchumi unaoanza kutekelezwa na baadhi ya wawekezaji ndani ya eneo hilo.

Mradi wa ujenzi wa Nyumba za kuuzwa kwa fedha taslimu na Mkopo uliopo eneo huru la Uchumi Fumba unatarajiwa kugharimu jumla ya Dola za Kimarekani Milioni Mia Moja na Ishirini { U$ Dollar 120,000,000 }.

Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
15/8/2015.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link