Home » » BREAKING NEWS: Profesa Lipumba ajiuzulu rasmi Uenyekiti CUF

BREAKING NEWS: Profesa Lipumba ajiuzulu rasmi Uenyekiti CUF

Written By CCMdijitali on Thursday, August 6, 2015 | August 06, 2015


Profesa Lipumba akizungumza na waandishi wa habari leo wakati akitangaza kujiuzulu.

MWENYEKITI wa Chama cha Wananchi CUF, Profesa Ibrahim Lipumba amejiuzulu rasmi wadhifa wake huo ndani ya chama kwa kikle alichokitaja kuwa ni kukiukwa kwa Katiba ya chama hicho.

Akizungumza na waandishi wa habari katika Hoteli ya Peacock jijini Dar es Salaam, Profesa Lipumba amesema  UKAWA ilianzishwa kwa lengo la kusimamia rasimu ya katiba mpya kutokana na maoni ya wananchi "sasa wenzetu wamegeuza UKAWA kwa kuleta mtu ambaye alishiriki kupitisha katiba pendekezwa ambayo siyo maoni ya wananchi hivyo kiongozi atakayeshinda kupitia UKAWA hawezi kusimamia maoni ya wananchi ya rasimu iliyopendekezwa na Warioba," amesema Lipumba.

Cha ajabu ni kwamba wakati wa vikao vya kumpitisha Lowassa kuwa mgombea wa Ukawa, Profesa Lipumba alikuwepo na ndiye aliyetoa taarifa kuhusu ujio wa Lowassa, hivyo taarifa hii inakinzana na kile alichokisema hapo awali.

Kujiuzulu huko kunahitimisha wasiwasi wa muda sasa ndani ya chama chake kuhusu hatima yake kutokana na sababu ambazo hazikujulikana mara moja. Profesa Lipumba alichaguliwa kuwa mwenyekiti wa chama mwaka 1999 na kugombea urais katika vipindi vinne ambavyo vyote alishindwa.

Tutawaletea habari kamili hivi punde.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link