Home » » Kimbisa: Sijahama na sitahama CCM

Kimbisa: Sijahama na sitahama CCM

Written By CCMdijitali on Monday, August 10, 2015 | August 10, 2015

Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dodoma Mheshimiwa Adam Kimbisa akihutubia wakazi wa Kibakwe kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Stendi ya Kibakwe


MWENYEKITI wa CCM mkoa wa Dodoma, Adam Kimbisa amekanusha uvumi kuwa ameungana na wenyeviti wengine wa mikoa wa CCM kukihama chama tawala nchini. 
Amesema wanaomzushia washindwe na walegee, kwani moyo na mwili wake upo CCM na kwamba kamwe hawezi kuhama.
Aliyasema hayo jana mjini hapa kutokana na kuwapo kwa taarifa amekihama chama hicho. Awali, jana kulikuwa na taarifa za Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Arusha, Onesmo ole Nangole kuhamia Chadema, kama ilivyokuwa kwa Mgana Msindai, aliyekuwa Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Singida aliyetangulia Chadema wiki iliyopita baada ya kushindwa kura za maoni ndani ya CCM.

Katika kuthibitisha hayo, Kimbisa jana alikuwa akiendesha vikao vya Kamati ya Siasa ya Mkoa akiwa katika sare zake za chama. Taarifa hizo zimekuja huku Kimbisa akiwa na habari nyingine katika gazeti hili (ukurasa wa 21) akielezea kushangazwa na wanaokihama chama baada ya kushindwa katika michakato ya kuwania uongozi, huku akisema kamwe yeye hawezi kufanya hivyo.

“Mwaka 2010 niligombea ubunge Jimbo la Dodoma Mjini nikahesabu kura zangu mwenyewe nyumbani nikajiona nimeshinda nikalala, asubuhi nilipoamka kumbe wagombea wenzangu wakaunganisha matokeo yao mgombea mmoja akaonekana ameshinda, lakini bado sikuhama na hadi leo nina damu ya kijani.

“Mtu akihangaika kuondoka CCM baada ya kushindwa tutamfuata hukohuko na tutampiga kwa kura tu,” alisisitiza Kimbisa.

 Na Mwandishi Wetu, Dodoma - Habari Leo
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link