Home » » Philemon Mollel - MONABAN achukua fomu ya NEC ,Jimbo la Arusha mjini.

Philemon Mollel - MONABAN achukua fomu ya NEC ,Jimbo la Arusha mjini.

Written By CCMdijitali on Friday, August 14, 2015 | August 14, 2015


MGOMBEA Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM) ,Ndg Philemon Mollel akipokea fomu za NEC ,kutoka kwa Mkurugenzi wa Uchaguzi Halmashauri ya Jiji la Arusha Ndg Juma Iddy leo.

Na  Veronica Mheta, Arusha

MGOMBEA Ubunge kupitia Chama cha Mapinduzi (CCM)  ,Philemon  Mollel amesema kuwa wanaohama CCM  ni utashi wao  na upo ndani ya dhamira yao lakini chama hicho kinauhakika wa kushinda Ubunge Arusha Mjini.

Aidha amesema atahakikisha anashirikiana na wananchi katika kuleta maendeleo  sambamba na kuwainua vijana , kinamama  pamoja na wazee katika kupambana na umaskini.

Monaban ambaye anajulikana kwa jina hilo maarufu aliyasema hayo jana Jijini hapa wakati alipokuwa akichukua fomu ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC)kwaajili ya kujaza taarifa zake na kuhakikiwa na Msimamizi wa Uchaguzi Jimbo la Arusha Mjini ,Juma Idd kabla ya Agosti 21 mwaka huu na Agosti 22 ndio mwisho wa uhakiki wa Nec.

Alisema yeye ambaye CCM imempitisha kupeperusha bendera ya chama hichohatishwi na wanaccm kukihama chama kwani ni utashi wao lakini alitamba ya kuwa CCM ipo imara .

“CCM ipo imara na haiwezwi kutishwa na hao wanaokihama chama nashukuru kwa kuchaguliwa kuwania ubunge na chama change hapa Arusha naahidi kuwatumikia wananchi utumishi unaotukuka”.

Alisema atajenga dira  ya maendeleo na kusimamia haki ,kuimarisha mahusiano na mawasiliano ya karibu na wapigakura pamoja na vyama vya upinzani sambamba na kutoa mikopo kwa vijana ,kinamama kwa kata zote 25 pamoja na kuwezesha wazee kupata bima ya afya kwaajili ya matibabu ikiwemo suala zima la elimu na nk.

Naye Katibu wa CCM Wilayani ya Arusha, Feruz Bano  aliongeza kuwa watazingatia maelekezo yaliyotolewa na NEC  ikiwemo kurejesha fomu hizo mapema.

Naye Msimamizi wa Uchaguzi , Idd alisema mgombea anatakiwa kujaza fomu hizo kwa umakini na kuzirudisha siku tatu kabla ya Agosti 21 mwaka huu na watabandika taarifa za wagombea kwa kila vyama huku kampeni zikianza rasmi  Agosti 22 mwaka huu.

Mwisho.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link