Home » » Balozi Seif azungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi, Kijiji cha Kiwani – Michakweni

Balozi Seif azungumza na Wanachama wa CCM na Wananchi, Kijiji cha Kiwani – Michakweni

Written By CCMdijitali on Monday, September 14, 2015 | September 14, 2015

Vijana Zuhura na Safi wakighani utenzi murua uliotoa burdani safi wakati wa hafla ya 
uzinduzi wa Balozi Seif Maskani ya Vijana wa CCM wa Kijiji cha Kiwani Michakweni.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Balozi Seif akizindua Maskani ya CCM ya Vijana wa
 Jimbo la Kiwani Wilaya ya Mkoani Mkoa wa Kusini Pemba iliyopewa jina lake.
 Balozi Seif akipandisha Bendera ya Maskani ya CCM ya Vijana wa Kiwani Iliyopewa jina la 
Balozi Seif Maskani mara baada ya kuizindua rasmi katika sherehe iliyofanyika Jimboni humo.
 Baadhi ya wanachama wa CCM na Wsananchi wa Kijiji cha Kiwani Michakweni wakifuatilia Hotuba ya Balozi Seif hayupo Pichani wakati wa uzinduzi wa Maskani ya Jina wa 
Kijiji hicho iliyopewa jina lake.
 Balozi Seif akisalimiana na Sheikh Faki Mohammed Khamis ambae ni mlemavu asiyeona
 baada ya kusoma Quran Tukufu wakati wa uzinduzi wa Balozi Seif Maskani hapo 
Kiwani Wilaya ya Mkoani.
 Vijana wa Maskani ya CCM ya Balozi Seif iliyopo Kiwani wakitoa burdani ya nyimbo maalum iliyoanikiza katika uzinduzi wa Maskani yao waliyoamua kuipa jina la Balozi Seif Maskani.
 Kaimu Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM Shaka Hamdu Shaka akiwakumbusha Vijana wa Kiwani Michakweni kuelewa wajibu wao wa kuhakikisha CCM Inaendelea kushika dola kwa kuwapa ushindi wagombea wa Chama hicho.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Balozi Seif Ali Iddi 
akizungumza na Wanachama wa CCM wa Jimbo la Kiwani mara baada ya kuizindua 
Balozi Seif Maskani ya Kijiji hicho.
Haiba ya Jengo la Balozi Seif Maskani liliopo Kiwani Kichakweni lililojengwa kwa kuzingatia 
Utamaduni wa Visiwa vya Zanzibar.
Picha na – OMR – ZNZ.

 Press Release:-

Mjumbe wa Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya Taifa ya 
Chama cha Mapinduzi Balozi Seif Ali Iddi amewaasa Wanachama wa Vyama vya upinzani Kisiwani Pemba kuacha kuendelea kukumbatia Viongozi ambao tayari wameshaonyesha
 muelekeo wa kutokubali kusimamia maendeleo yao kwa zaidi ya 
miaka Ishirini sasa.

Alitoa nasaha hizo wakati akizungumza na Wanachama wa
 Chama cha  Mapinduzi { CCM } na Wananchi wa Kijiji cha Kiwani – Michakweni Jimbo la Kiwani mara baada ya 
kuizindua Rasmi Maskani ya  Vijana wa CCM wa Jimbo hilo iliyopewa Jina lake.

Balozi Seif alisema wakati wa kuacha kudanganywa kwa sera na ahadi zisizotekelezeka za Viongozi hao wanaojali 
maslahi yao binafsi umefika kwa wafuasi hao wa Upinzani
 na badala yake wajiunge na Chama cha Mainduzi kabla hawajaachwa njia panda.

Alisema Gari la Chama cha Mapinduzi hivi sasa bado linaruhusu
kupakiwa abiria wowote watakaoamua kutoka vyama 
vya upinzani ambao wanaonekana kuchoshwa na vitendo vinavyoviza Maendeleo yao kwa kiindi kirefu sasa.

Balozi Seif alielezea faraja yake kutokana na Wananchi walio wengi
Kisiwani Pemba kuonyesha dalili za kuchoshwa na hatimae kukataa
Viongozi wasiojali Maendeleo ya Wananchi.

Mjumbe huyo wa Kamati Kuu ya CCM Taifa alisema 
katika kuuzika upinzani
katika Uchaguzi Mkuu ujao wa mfumo wa Vyama vingi vya Siasa
aliwakumbusha Wana CCM waendelee kushikamana lengo 
likiwa ni kumaliza upinzani huo usio na muelekeo wa Maendeleo.

Amewapongeza Vijana hao wa Balozi Seif Maskani wa 
Kiwani Michakweni
kwa uamuzi wao wa kujenga Jengo lililozingatia Utamaduni wao na
kuwaahidi kusaidia kuiimarisha katika kiwango kinacholingana na Chama chenyewe.

Alisema msaada huo utakwenda sambamba na kuzingatia 
mipango imara ya kuwapatia Boti ya uvuvi itakayowapa fursa ya kujiajiri wenyewe ili waweze kukidhi mahitaji yao ya Kimaisha.

Balozi Seif alieleza kwamba tabia ya kukaa vijiweni hivi sasa imepitwa na wakati kulingana na mabadiliko ya mfumo wa Dunia uliopo hivi sasa ambao unamkaba mwanaadamu lazima afanye kazi.

Akitoa Taarifa fupi ya Vijana hao wa Balozi Seif Maskani Mmmoja wa Viongozi wa Maskani hiyo Ndugu Mohammed Juma alisema Maskani hiyo imeasisiwa Mwaka 2014 ikianza na Wanachama 22 na hivi sasa imeongeza wanachama na kufikia 36.

Nd. Mohammed alisema kwamba Vijana hao wamejipanga kuwa Maskani ya chuo cha Vijana katika kuwafundisha sera za Chama cha Mapinduzi pamoja na Itikadi zake zitakazosaidia Vijana hao kuelewa Historia ya Taifa hili lililojikomboa 
kutokana na madhila ya wakoloni.

Vijana hao wa Balozi Seif Maskani Kiwani Michakweni wameupongeza Uongozi wa Serikali ya Wilaya ya Mkoani kwa kuwahakikishia usalama licha ya vitisho wanavyoendelea kufanyiwa na wafuasi wa Upinzani kwa
uamuzi wao wa kuunga mkono Chama cha Mapinduzi.

Naye akisalimia na Vijana hao wa Balozi Seif Maskani ya Kiwanchi
Michakweni Mke wa Mjumbe huyo wa 
Kamati Kuu ya CCM Taifa Mama Asha Suleiman Iddi amewataka akina Mama wa Kijiji na Jimbo hilo kuhakikisha
kwamba Viongozi watakaowachaguwa wawe tayari kufanya nao kazi pamoja.

Mama Asha alisema wapo viongozi wenye tabia ya kwenda Majimboni kuomba kura na baadaye kuwatelekeza Wananchi hao bila ya kujali kwa vitendo vyao vya kutafuta maslahi katika maeneo mengine vinawanyima haki Wananchi wao.
 Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
14/9/2015.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link