Home » , » Dk. Wilbroad Slaa awalipua UKAWA na Lowassa.

Dk. Wilbroad Slaa awalipua UKAWA na Lowassa.

Written By CCMdijitali on Tuesday, September 1, 2015 | September 01, 2015


 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa pia amesema kuwa mambo yaliyotokea katika chama chake ndio maana ameamua kuachana na siasa rasmi hii leo.
 Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa akizungumza na waandishi wa habari katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam leo, baada ya kukaa kimya kingi sana tangu mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo chini ya mwamvuli wa UKAWA, Edward Lowassa kuhamia chama hicho. 

Leo ameibuka na kusema ya moyoni kuwa amejivua uanachama rasmi wa chama cha Chadema pamoja na Ukatibu Mkuuu wa Chama cha hicho na kuaachana kabisa na siasa kutokana na mambo yaliyokuwayakifanyika ndani ya chama chake hayakumlidhisha na hakukubaliana nayo.
 Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa katika harakati za kupata taswira nzuri za Aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA, Dk. Wilbroad Slaa katika mkutano uliofanyika katika hoteli ya Serena jijini Dar es salaam leo
Baadhi ya wananchi pamoja na waandishi wa habari wa vyombo mbalimbali vya habari wakimsikiliza aliyekuwa Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo Dk. Wilbroard Slaa leo katika hoteli ya Serena jijini Dar es Salaam.


Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link