Home » » MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA MAGUFULI, KUMSIKILIZA RUVUMA.

MAELFU YA WATU WAJITOKEZA KUMSIKILIZA MAGUFULI, KUMSIKILIZA RUVUMA.

Written By CCMdijitali on Tuesday, September 1, 2015 | September 01, 2015


Mgombea urais wa Tanzania kupitiaa CCM,, dK John Magufuli akiwa na watoto aliowapatia zawadi alipokuwa akiondoka baada ya kujinadi katika Jimbo la Peramiho, mkoani Ruvuma. 
 Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli akiwasalimia wananchi wa Songea waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Maji Maji mjini humo mkoani Ruvuma,Mgombea huyo ambaye anawaomba Watanzania ridhaa ya kuwaongoza katika awamu ya tano.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia umati wa wakazi wa mji wa Songea, ambapo alisema katika serikali yake wakulima hawatokopwa mazao yao, mbolea zitapatikana kwa wakati, barabara zitaboreshwa ,elimu bure mpaka kidato cha nne, kuongeza maslahi ya walimu pamoja na kuboresha huduma za afya.

Mgombea Ubunge Jimbo la Peramiho, Jenista Mhagama akipokea Ilani ya Uchaguzi ya CCM kutoka kwa Mgombea Urais kupitia chama hicho, Dk Magufuli wakati wa mkutano huo wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha mkoani Ruvuma.
 Dk Magufuli akimnadi Mgombea Ubunge wa CCM Jimbo la Nyasa, Stelah Manyanya katika mkutano wa kampeni katika Mji wa Lituhi,ambapo pia alimkabidhi Ilani ya chama hicho.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akimkabidhi mgombea ubunge wa Jimbo la Mbinga Ndugu Sixtus Mapunda kitabu cha Ilani ya Uchaguzi ya CCM kwenye mkutano wa hadhara uliofanyika Mbinga mjini.
 Dk Magufuli akishuka kwenye Kivuko cha Mto Ruhuhu akitokea Wilaya ya Ludewa Mkoani Njombe kwenda Mbinga mkoani Ruvuma kuendelea na kampeni za urais ubunge na udiwani. Dk Magufuli ameahidi kujenga daraja la mto huo.
 Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM,Dkt John Pombe Magufuli akizungumza jambo na mkazi wa mji wa Peramiho ambaye ni mlemavu wa ngozi,jioni ya leo mara baada ya kumaliza kuwahutubia wananchi wa mji huo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Dk Magufuli akimsalimia mmoja wa walemavu waliojitokeza kwenye mkutano wa kampeni mjini Mbinga.
 Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCm Dk. Emmanuel Nchimbi akihutubia wakazi wa Songea mjini ambapo aliwataka wananchi hao kumpa kura nyingi Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli kwenye uchaguzi utakaofanyika Oktoba 25,kwa sababu ni Muaminifu,muadilifu na ni mchapa kazi.
 Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi ambaye pia ni mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM Taifa Ndugu William Lukuvi akihutubia wakazi wa Songea mjini kwenye mkutano wa kampeni za CCM uliofanyika kwenye uwanja wa Maji Maji jioni ya leo.
 Maelfu ya Wananchi wakiwa wamefurika ndani ya uwanja wa maji maji mjini Songea jioi ya leo kwenye mkutano wa kampeni wa CCM,mkoani Ruvuma jioni ya leo,ambapo Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe aliwahutubia wananchi hao.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa Mbinga.
 Wananchi wakifuatilia hotuba ya Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli katika mkutano wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Tamasha-Peramiho mkoani Ruvuma jioni ya leo.
 Wananchi wakishangilia
 Umati wa wakazi wa Peramiho wakisikiliza hotuba ya Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli wakati wa mkutano wa kampeni katika uwanja wa Tamasha ndani ya jimbo la Peramiho mkoani Ruvuma.
 Baadhi ya Wananchi wa Peramiho wakifurahia jamo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
 Mgombea wa Urais kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM)Dk. John Pombe Magufuli akiwaaga wakazi wa Mbinga.
 Wananchi wakishangilia jambo kwenye mkutano wa kampeni za ccm leo jioni ndani ya uwanja wa Maji Maji mjini Songea.

Wananchi wa Songea mjini wakishangilia jambo wakati mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia chama cha CCM Dkt John Pombe Magufuli alipokuwa akiwahutubia katika mkutano wa kampeni kwenye uwanja wa Maji maji mjini humo.
PICHA ZOTE NA MICHUZI JR-RUVUMA
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link