Home » » DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO YA WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUDUMU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) NA WATAALAMU WA HAKI NA SHERIA, JIJINI ARUSHA

DKT. BILAL AFUNGUA MKUTANO WA MASHAURIANO YA WAWAKILISHI WA KAMATI YA KUDUMU YA UMOJA WA AFRIKA (AU) NA WATAALAMU WA HAKI NA SHERIA, JIJINI ARUSHA

Written By CCMdijitali on Thursday, September 3, 2015 | September 03, 2015

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Afrika( AU) wakati alipokuwa akiwasili kwenye Hoteli ya Mount Meru Jijini Arusha kwa ajili ya kufungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli hiyo uliokuwa ukijadili kuhusu kuimarisha demokrasi, utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi. Wa tatu (kulia) ni Jaji Mkuu Mstaafu Agustino Ramadhan..

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akihutubia wakati akifungua Mkutano wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu kuimarisha demokrasi, utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.

 Baadhi ya washiriki wa Mkutano huo wakimsikiliza Makamu wa Rais, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, wakati akihutubia.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akiteta jambo na Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu kuimarisha demokrasi, utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal (kulia) akikabidhiwa zawadi na Rais wa Mahakama Afrika Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakati wa ufunguzi wa Mkutano huo wa Mashauriano kati ya Wawakilishi wa Kamati ya Kudumu ya Umoja wa Afrika( AU) na Wataalamu wa Masuala ya Haki na Sheria, uliofanyika kwenye Hoteli ya Mount Meru jijini Arusha jana Sept 2, 2015 ambao ulikuwa ukijadili kuhusu kuimarisha demokrasi, utawala wa sheria na masuala ya uchaguzi.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na Rais wa Mahakama ya Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu wa Tanzania, Agustino Ramadhan, wakisalimiana na baadhi ya washiriki wa mkutano huo baada ya kufunguliwa rasmi jana jijini Arusha.

 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Rais wa Mahakama Afrika, Jaji Mkuu Mstaafu, Agustino Ramadhan, wakiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya washiriki wa mkutano huo kutoka mataifa mbalimbali ya Afrika baada ya ufunguzi jana jijini Arusha. Picha na OMR
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link