Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli,akiwahutubia Wananchi wa Tabora jioni ya leo kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni uliofanyika katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi.Dkt Magufuli alisema kuwa Serikali yake kwa sehemu kubwa itakuwa upande wa wananchi wanyonge ili hatimaye wawe na maisha yenye neema na kwenye hilo ana uhakika atafanya kazi nzuri maana kwake yeye ni kazi tu na hakuomba kuwa Rais ili awe mwanasiasa bali anaomba nafasi hiyo kwa kujua anajua namna ambavyo amejipanga kufanya kazi kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania wote.
Sehemu ya umati wa watu waliokuwa katika uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo walipokuwa wakimsikiliza Mgombea Urais wa CCM Dkt Magufuli.
Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Abdulrahman Kinana akihutubia wakazi wa tabora mjini na kuwaambia kuwa Dk. Magufuli ni kiongozi sahihi anayehitajika Tanzania kwa sasa na kuwataka wananchi kumpigia kura zote ifikapo Oktoba 25 mwaka huu.
Mmoja wa Makada walioko kwenye timu ya uhamasishaji wa kampeni za CCM,Mh.Samweli Sitta akiwahutubia wananchi wa Tabora kwenye mkutano wa kampeni za Urais ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi jioni ya leo.
Mgombea wa Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Chama Cha Mapinduzi Dk. John Pombe Magufuli akihutubia wakazi wa mji wa Tabora waliofurika kwenye mkutano wa kampeni za CCM ambapo aliwaambia anataka kujenga Tanzania mpya yenye kuleta maendeleo kwa wananchi wote.
Mgombea Urais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,kupitia chama cha Mapinduzi (CCM),Dkt John Magufuli akiwapungia mkono wananchi wa mji wa Tabora waliokuwa wamefurika kwenye uwanja wa Ali Hassa Mwinyi mapema leo jioni,alipokuwa akiwasili kwenye mkutano wa hadhara wa kampeni.
Wafuasi wa chama cha CCM wakiwa na Mabango yao ndani ya uwanja wa Ali Hassan Mwinyi,wakimpokea Mgombea Urais wa CCM Dkt John Pombe Magufuli
Mgombea urais wa CCM Dk.John Magufuli aliyevaa kofia akizungumza jambo na Mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega Mjini,Ndugu Hussein Bashe(katikati) na Mgombea Ubunge jimbo la Nzega Vijijini Dk.Hamis Kigwangala mchana wa leo walipokuwa kwenye mkutano wa kampeni za urais uliofanyika Uwanja wa Barafu wilayani Nzega mkoani Tabora
Mgombea Ubunge jimbo la Nzega Vijijini Dk.Hamis Kigwangala akiwasalimia wananchi wa Nzega mchana wa leo walipokuwa kwenye mkutano wa kampeni za urais uliofanyika Uwanja wa Barafu wilayani Nzega mkoani Tabora
Mgombea Ubunge wa jimbo la Nzega Mjini,Ndugu Hussein Bashe akiwahutubia wananchi walipokuwa kwenye mkutano wa kampeni za urais uliofanyika Uwanja wa Barafu wilayani Nzega mkoani Tabora.
MMoja wa Makaba wa CCM ambaye yupo kwenye orodha ya timu ya kampeni ya kumnadi Mgombea Urais wa chama hicho Dkt John Magufuli,Stephen Masele akiwahutubia wananchi mapema leo mchana kwenye mkutano wa kampeni.
Wananchi wakishangilia wakati Dkt Magufuli alipokuwa akiwahutubia
Wananchi wakiwa katika mkutano wa kampeni wa Dk John Pombe Mgufuli mjini Tabora hii leo.