Home » » KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA CHAENDESHA SEMINA JIJINI ARUSHA

KITUO CHA DEMOKRASIA TANZANIA CHAENDESHA SEMINA JIJINI ARUSHA

Written By CCMdijitali on Sunday, September 13, 2015 | September 13, 2015

Taasisi ya Vyama Vingi ya Uholanzi (Netherlands Institue for Multiparty Democracy) ikishirikiana na Kituo Cha Demokrasia Tanzania (TCD) kimeendesha mafunzo ya siku mbili Jijini Arusha, kwa Vyama vya Siasa Mkoani Arusha  kwa ajili ya Wakufunzi wa Mawakala wa Vyama 
11-12/09/2015 katika Hoteli ya Savoury:
  • Umuhimu wa Uadilifu katika Uchaguzi

  • Sababu za kuwa na Mawakala wa Vyama wakati wa Uchaguzi

  • Mifano ya Matukio Yanayoweza Kukinzana na Maslahi ya Wagombea

  • Vifungu vya Sheria za Tanzania vinavyohusu mawakala wa Vyama

  • Haki na wajibu wa Mawakala

  • Usalama wa Kituo cha Kupigia Kura Siku ya kupiga na Kuhesabu Kura

  • Mpangilio wa Kituo cha Kupigia Kura siku ya Kuhesabu Kura

  • Mchakato wa Upigaji Kura Kuanzia kituo Kinapofunguliwa mpaka kinapofungwa

  • Kuhesabu, Majumuisho na Maandalizi ya Karatasi za Matokeo ya Kuara

  • Aina gani ya ushahidi Unakubalika Wakati wa Mchakato wa Upigaji Kura

  • Kuzifahamu baadhi ya Fomu muhimu kwa Mawakala wa Vyama vya Siasa

Mafunzo hayo yaliendeshwa na:
  • Bi Consolata Sule ,Mratibu wa  Mikoa ya (Arusha, Manyara, Morogoro na Tanga) Kituo cha Demokrasia Tanzania.

  • Bi Laetitia Petro- Mwanaharakati na Mwanasheria

  • Bwn Charles Rwekaza , Mhadhiri wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania


  Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi Bi Esther Maleko akichora mchoro kuonyesha mpangilio wa Kituo cha Kupigia kura Siku ya kupiga kura na kuhesabu kura.


  Mkufunzi wa mafunzo Bi Laetitia Petro- (Mwanaharakati na Mwanasheria) akifuatilia jambo katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa katika Hoteli kwa jina maarufu Savoury Hotel ya Jijini Arusha.
 Bi Consolata Sule ,Mratibu wa Mikoa ya (Arusha, Manyara, Morogoro na Tanga) Kituo cha Demokrasia Tanzania akifanya mawasiliano katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa katika Hoteli kwa jina maarufu Savoury Hotel ya Jijini Arusha.
Baadhi ya  Washiriki kutoka Vyama mbali vya Siasa , kwa mujibu wa taratibu za Kituo cha Demokrasia Tanzania.
 Baadhi ya Washiriki kutoka Vyama mbali vya Siasa , kwa mujibu wa taratibu za Kituo cha Demokrasia Tanzania.

 Baadhi ya Washiriki kutoka Vyama mbali vya Siasa , kwa mujibu wa taratibu za Kituo cha Demokrasia Tanzania.
 Baadhi ya Washiriki kutoka Vyama mbali vya Siasa , kwa mujibu wa taratibu za Kituo cha Demokrasia Tanzania.
 Wawakilishi kutoka cha cha Chadema .


 Kushoto - Kulia ni Bwn Charles Rwekaza , Mhadhiri wa Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania na Bi Laetitia Petro- (Mwanaharakati na Mwanasheria) akifuatilia jambo katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa katika Hoteli kwa jina maarufu Savoury Hotel ya Jijini Arusha.

 Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi Bi Esther Maleko akitoa maaelezo juu ya mchoro   unao onyesha mpangilio wa Kituo cha Kupigia kura Siku ya kupiga kura na kuhesabu kura.
 Mwakilishi wa Chama Cha Mapinduzi Bi Aisha Mbaraka akitoa maaelezo juu ya mchoro unao onyesha mpangilio wa Kituo cha Kupigia kura Siku ya kupiga kura na kuhesabu kura.


 Baada ya mafunzo , viongozi wakibadilishana mawazo .
Picha na Jasper Kishumbua- Arusha

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link