Home » » Mgombea Ubunge wa CCM Arusha ,afariji familia zilizopoteza mali kwa kuunguliwa na moto leo.

Mgombea Ubunge wa CCM Arusha ,afariji familia zilizopoteza mali kwa kuunguliwa na moto leo.

Written By CCMdijitali on Monday, September 28, 2015 | September 28, 2015

Ndg Philemon Mollel na mgombea Ubunge wa CCM Wilaya ya Arusha, ametembelea familia tatu zilizopoteza mali zao kwa kuunguliwa na moto ,usiku wa kuamkia leo majira ya saa 7.00 usiku, mtaa wa Suye, Kata ya Olorieni ya Jijini Arusha.
  • Familia 2 ,mojawapo ya  Bi Daishi Wilson Urio na mwingine ambaye hatukuweza kupata jina lake wamepoteza mali zao zote ,kwani hawakuweza kuokoa chochote. 
  • Familia ya Bi Nana Lotuno - mfanyakazi wa School of International Training ya Jijini Arusha ,ilifanikiwa kuokoa baadhi ya vitu na baadhi kuteketea kabisa.
  • Familia zote sasa hivi zinaishi kwa majirani ,kutokana na moto huo kuathiri sehemu kubwa ya paa la nyumba.
Ndg Philemon Mollel mara  baada ya kutembelea eneo la tukio, ametoa msaada wa 
Bati 50,
  • Unga wa ngano na mahindi katoni tano kila moja,
  • Mafuta ya kupikia lt 20 
  • Fedha taslimu Tz  sh 200,000/= kwa ajili ya kujikimu vitu vya msingi.
  • Msaada huo aliukabidhi kwa Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Serekali ya Mtaa wa Suye Ndg Zakaria Muro.

SHUKURANI:

Ndg Zakaria Muro Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Suye ,amemshukuru Ndg Philemon Mollel
 ( Mgombea Ubunge wa CCM Wilaya ya Arusha) pamoja na msafara wa Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Wilayani hapo waliokuwa wameambatana na mgombea huyo akiwemo Mwenyekiti wa CCM Wilaya ,Ndg Wilfred Soilel , Katibu wa Siasa na Uenezi CCM (W), Ndg Jasper Kishumbua,Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya,Ndg Martin Munis  na Katibu wa CCM Kata ya Olorien Ndg Jonas Daudi  akiwa amefuatana na Mgombea Udiwani Kata hiyo Ndg Mosses Koye, kwa niaba ya wananchi wa Mtaa wa Suye. Aidha amewataka viongozi wengine na Taasisi nyingine  kujitokeza,kusaidia familia hizo kwa kupitia kamati ndogo ya Maafa,iliyoundwa leo katika Ofisi ya Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Suye na kusema kuwa "Hiyo ndiyo Ibada ya kweli kwa msaada walioutoa"
 Mbunge mteule wa CCM Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel akikagua sehemu ya nyumba iliyoathiriwa na moto , leo asubuhi.


 
 Sehemu ya nyumba iliyoathiriwa na moto.
 
 Mbunge mteule wa CCM Jimbo la Arusha Ndg Philemon Mollel akikagua sehemu ya nyumba iliyoathiriwa na moto , leo asubuhi.
 
 Sehemu ya nyumba iliyoathiriwa na moto.
 Katikati ni Ndg Zakaria Muro ,Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Suye akishukuru kwa msaada uliotolewa na   Ndg Philemon Mollel ( Mgombea Ubunge wa CCM Wilaya ya Arusha) (aliyevaa koti) na aliyevaa kofia ni Katibu wa CCM Kata ya Olorien Ndg Jonas Daudi ,katika eneo la ajali.
 Mmiliki wa nyumba hizo Ndg joseph Mmasy akiwa katika eneo la tukio, leo.
 Ndg Philemon Mollel ( Mgombea Ubunge wa CCM Wilaya ya Arusha) akimfariji  Bi Daishi Wilson Urio, aliyepoteza mali zake zote katika janga hilo la moto.
Ndg Zakaria Muro ,Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Suye akitoa neno la shukrani mara baada ya kupokea  msaada uliotolewa na Ndg Philemon Mollel ( Mgombea Ubunge wa CCM Wilaya ya Arusha).
 
 Ndg Philemon Mollel ( Mgombea Ubunge wa CCM Wilaya ya Arusha) akimfariji Bi Nana Lotuno  Urio, aliyepoteza mali zake zote katika janga hilo la moto.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha - Ndg Jasper Kishumbua.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link