Shamsi azindua kampeni ya uchaguzi Jimbo la Mahonda kwa tiketi ya CCM
Written By CCMdijitali on Friday, September 18, 2015 | September 18, 2015
Labels:
KITAIFA
#Kaziiendelee
Kaulimbiu | Desemba 09,2016“Tuunge mkono jitihada za kupinga rushwa na ufisadi na tuimarishe uchumi wa viwanda kwa maendeleo yetu.”
Miaka 55 ya Uhuru wa Tanzania Bara
Wa kwanza kutoka Kulia ni Balozi Seif Ali Iddi anayegombea nafasi ya Uwakilishi, Mh. Bahati Ali Abeid nafasi ya Ubunge, Nyuma ya Balozi Seif ni Bibi Hadia Juma Chumu nafasi ya Udiwani Wadi ya Fujoni na Nyuma ya Mh. Nahodha ni d.
Haji Fadhil Udiwani Wadi ya Mahonda.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Mh. Shamsi alisema hayo wakati akiizundua kampeni ya uchaguzi Jimbo la Mahonda kwa tiketi ya CCM iliyozinduliwa kwenye uwanja wa Michezo wa Kazole Wilaya ya Kaskazini “ B”.
Alisema wakati huu wa kampeni zinazoendelea ni muhimu kwa wanachama wa chama cha Mapinduzi kupata Viongozi makini watakaokuwa na uwezo wa kusimamia maendeleo yao kwa haraka.
Mh. Nahodha ambae pia ni Waziri Kiongozi Mstaafu wa Zanzibar alieleza kwamba zipo sera za uongo zinazoendelea kutangazwa katika mikutano ya kampeni inayoendelea ambazo zinaonyesha wazi kwamba hazitekelezeti.
Alitahadharisha kwamba Wana CCM na Wananchi wote wana kazi kubwa ya kuhakikisha kuwa Mapinduzi matukufu ya Zanzibar ya Mwaka 1964 yanalindwa kwa gharama yoyote ile kwa vile zipo sera za baadhi ya vyama vya siasa zinazoonyesha wazi kupinga Mapinduzi hayo.
Alisema wananchi wasifikiri kwamba maadui wa Mapinduzi bado wapo na zipo dalili zinazoonyesha wapinga mapinduzi wataendelea kuzaliwa ndani ya nje ya Taifa hili.
Akifafanua sera na ilani za Chama cha Mapinduzi zinazotarajiwa kutekelezwa katika miaka mitano ijayo endapo Wazanzibari wataipa fursa CCM kuendelea kuondoza dola katika uchaguzi Mkuu wa Mwezi ujao Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imekusudia kuendelea kujenga Bara bara zenye urefu wa Kilomita 160 Unguja na Pemba.
Hatua hiyo ina lengo la kujenga miundombinu ya mawasiliano ya bara bara ili kuimarisha sekta ya Uchumi kama Utalii na Kilimo jambo ambalo litasaidia kunyanyua uchumi wa Taifa sambamba na kupunguza umaskini kwa wananchi walio wengi hasa Vijijini.
Mh. Nahodha aliipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar chini ya Uongozi wa Rais wa Sasa anayemaliza muda wake Dr. Ali Mohammed Shein kwa kazi kubwa iliyofanya katika kipindi cha miaka mitano inayomaliza sasa ya kuimarisha uchumi.
Alisema Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar imefanikiwa kuongeza pato la taifa na kupindukia kwa zaidi ya asilimia 7% sambamba na kupungusa mfumko wa bei uliowaa nafuu wananchi kukabiliana na ukali wa maisha.
Mapema Katibu wa Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Kaskazini “B “ Bibi Subira Mohammed Ali alisema utekelezaji makini wa sera za Chama cha Mapinduzi ndani ya Wilaya hiyo katika kipindi cha miaka mitano umeleta maendeleo makubwa ndani ya Wilaya hiyo.
Bibi Subira alisema utekelezaji huo ni kigezo tosha kinachothibitisha kwamba wagombea wa nafsi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani wa Majimbo ya Wilaya hiyo wana uwezo mkubwa unaostahiki kuzingatiwa na wapiga kura katika kuwachagua kuwaongoza.
Mjumbe huyo wa kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Mh. Shamsi Vuai Nahodha katika mkutano huo wa Kampeni alipata fursa za kuwanadi wagombea Uwakilishi, Ubunge na Wadi zilizomo ndani ya Jimbo Jipya la Mahonda.
Wagombea hao wa CCM ni Balozi Seif Ali Iddi mgombea Uwakilishi, Mh. Bahati Ali Abeid Nassir Nafasi ya Ubunge, Ndugu Hadi Juma Chum Wadi ya Fujoni na Nd. Haji Hadhil Wadi ya Mahonda.
Wakiomba kura wagombea hao wa CCM waliahidi kusimamia utatuzi wa changamoto zinazowakabili wananchi hasa huduma za kijamii kama Maji, Umeme pamoja na Elimu.
Walisema ushindi wa Chama cha Mapinduzi katika uchaguzi Mkuu wa mara hii haina mjadala kutokana sera nyepesi zinazotangazwa na wagombea nafasi tofauti wa vyama vya upinzani.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa 9ili wa Rais wa Zanzibar
18/9/2015.