Waziri Mkuu, Mizengo Pinda katikati akizungumza na wananchi waliofika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Felix Ntibenda ambaye yupo kushoto kwa waziri mkuu kwaajili ya kushuhudia ugawaji wa magari mawili ya wagonjwa(ambulance) zilizotolewa na Pinda kwaajili ya kuwasaidia wananchi wa Wilaya ya Ngorongoro kwa lengo la kupata huduma bora za afya,kulia kwake ni Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro, Hashimu Shaibu.
Waziri Mkuu akitoka kuangalia moja kati ya ambulance mbili alizozitoa kwaajili ya wakazi wa wilaya ya Ngorongoro.
Mmoja kati ya ambulance aliyoikabidhi kwa Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro,Hashimu Shaibu
Hapa akiangalia gai hilo lililokuwa likiwashwa na Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro, Hashimu Shaibu
Hapa kazi kazi tu ,hayo ni maneno ya RC, Felix Ntibenda na kusema asante mkuu kwa kutoa magari haya mawili baada ya kufanya ziara Septemba mwaka uliopita na kuona jinsi wanawake na watoto pamoja na wananchi wanavyoteseka kupata huduma za afya kutokana na mazingira ya Wilaya ya Ngorongoro
Naikabidhi rasmi na natimiza ahadi kwa wananchi wa Ngorongoro ya kuwapa magari ya wagonjwa
Waziri Mkuu Pinda akimwonyesha RC Ntibenda gari hilo la kisasa la kubebea wagonjwa
Hapa waziri Mkuu Pinda akikata utepe kwaajili ya kukabidhi ambulance hiyo, anayeshuhudia na RC ,Nyibenda pamoja na watumishi mbalimbali na wananchi ambao hawapo pichani
WAZIRI Mkuu ,Mizengo Pinda amekabidhi magari mawili ya wagonjwa
kwaajili ya kuwasaidia wananchi wa Vijiji vya Endulen na Waso ambao
walikuwa wakipta adha ya huduma ya afya kutokana na mazingira ya
kijografia yaliyopo Wilayani Ngorongoro Mkoani Arusha
Akikabidhi magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa Mkuu wa Mkoa wa Arusha,
Felix Ntibenda jana ,Pinda alisema ametoa msaada huo binafsi kutokana
na ziara yake ya kikazi aliyoifanya mwaka 2013 mwezi Septemba Wilayani
Ngorongoro na kuona adha wanayoipata wananchi wa wilaya hiyo katika
kupata huduma za afya.
Alisema alipokuwa katika ziara hiyo aliona jinsi wananchi wanavyofuata
huduma za afya mbali na maeneo wanayoishi sambamba na huduma za wamama
pale wanapohitaji kujifungua na aliombwa na wananchi wa wamaeneo hayo
ili awasaidie kupata magari kwaajili ya huduma za afya katika wilaya
hiyo.
“Nilipokuwa katika ziara yangu Ngorongoro niliona changamoto
mbalimbali za huduma ya afya na nikaahidi kuwasaidia na leo binafsi
nimetoa magari haya mawili ili yaweze kuwasaidia wananchi wa huko
katika kupata huduma bora na magari mengine yatakuja tunafanya
mawasiliano na Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii ili kuhakikisha
wilaya hiyo inakuwa na magari sanjari na huduma bora za afya”.
Aliongeza kuwa magari hayo mawili ambayo yananamba za usajili T759 DEP
na T865 DEC yametolewa kupitia kwa watanzania waishio Japan na
yamekuja kwaajili ya kuwezesha watanzania kupata huduma bora za afya
wilayani humo.
Naye Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Ntibenda alimshukuru Pinda kwa kutimiza
ahadi ya kuwasaidia wananchi wa wilaya hiyo kutokana na ziara
aliyoifanya wilayani humo.
Hata hivyo Mkuu wa Wilaya ya Ngorongoro Hashimu Shaibu alimshukuru
Pinda kwa msaada huo na kuongeza kuwa msaada huo umekuja wakati
muafaka kwani wilaya hiyo inachangamoto ya kijografia ya maeneo hivyo
magari hayo ni msaada mkubwa kwa wananchi wanaoishi wilayani humo.