Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi kati kati akiongoza matembezi ya kuadhimisha siku ya Sheria Zanzibar yalioanzia Mahakama Kuu Vuga Mjini Zanzibar na kuishia Viwanja vya Maisara.
Kulia ya Balozi Seif ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu na Kushoto yake ni Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar Mh. Said Hassan Said na Mkuu wa Wiulaya ya Kati Nd. Vuai Mwinyi.
Baadhi ya Vikundi vya mazoezi vikipasha mwili katika Viwanja vya Maisara Suleiman baada ya kukamilisha matembezi ya siku ya Sheria Zanzibar.
Baadhi ya Vikundi vya mazoezi vikipasha mwili katika Viwanja vya Maisara Suleiman baada ya kukamilisha matembezi ya siku ya Sheria Zanzibar.
Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu akijiandaa kumkaribisha Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif kuzungumza na washiriki wa matembezi ya Siku ya Sheria Zanzibar hapo Maisara Suleiman.
Kamanda wa Polisi Mkoa Mjini Magharibi Kamishna Msaidizi wa Polisi Mkadam Khamis Mkadam akiwa miongoni mwa wanakikundi cha mazoezi cha Ziwani walioshiriki matembezi ya siku ya Sheria akifuatilia kwa makini hotuba ya mgeni ramsi kwenye hafla hiyo.
Balozi Seif akizungumza na washiriki wa matembezi ya Siku ya Sheria Zanzibar yaliytoshirikisha watumishi wa sekta ya Sheria pamoja na vikundi vya mazoezi ya Vioungo Nchini hapo Maisara Suleiman.
Wa kwanza kutoka kulia ni Jaji Mkuu wa Zanzibar Mheshimiwa Omar Othman Makungu.

Balozi Seif akiagana na Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Makungu mara baada ya kumalizika kwa matembezi ya Siku ya Sheria Zanzibar wakishuhudiwa na Mwanasheria Mkuu wa SMZ Mh. Said Hassan Said mwanzo kulia.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Press Release:-
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi ametoa wito kwa Majaji na Mahakimu Nchini kuacha kugugumizi katika utoaji wa haki ili kuondoa au kupunguza zaidi muda mrefu unaochukuliwa na Majaji na Mahakimu hao katika kutoa hukumu kwa kesi zinazopelekwa Mahakamani.

Alisema kigugumizi hicho mbali ya kulalamikiwa kwa kipindi kirefu na Wananchi walio wengi lakini pia kinachangia sana kuuondolea Heshima yake Muhimili huo ukiwa miongoni mwa Mihimili Mitatu ya Dola.
Balozi Seif Ali Iddi alitoa wito huo wakati akizungumza na Majaji, Wanasheria na Mahakimu ndani ya Jumla la Sheria Zanzibar baada ya kuyaongoza Matembezi ya maadhimisho ya Siku ya sheria yaliyoanzia Mahakama Kuu Vuga kupitia Benbella, Michenzani, Kituo cha Polisi madema na kumalizikia katika Viwanja vya Michezo vya Maisara Mjini Zanzibar.
Alisema zipo kesi zinazolalamikiwa na Wananchi walio wengi kama Dawa za kulevya na udhalilishaji wa Kijinsia unaowakumba zaidi watoto wadogo na wanawake ambazo hupelekwa Mahakamani lakini hatma yake inaishia hewani na wahusika kuwaona wakiendelea kutanua mitaani.
Balozi Seif alieleza kwamba ushahidi wa wazi katika baadhi ya kesi zinazopelekwa kwa Mahakimu hutolewa na wahusika lakini kinachojitokeza kwa baadhi ya Majaji na Mahakimu kueleza kuwa ushahidi bado haujakamilika.
Katika kukabiliana na vitendo hivyo Balozi Seif amewakumbusha watendaji wa Mahakama kubeba jukumu lao kwa kuchukuwa hatua za haraka za kutoa maamuzi ili kupunguza mrundikano wa majalada ya kesi yaliyopo mezani kwao.
“ Majaji na Mahakimu wanapaswa kujiepusha na malalamiko ya mrundikano wa mashauri yanayowahusu ambayo yamekuwa yakilalamikiwa sana na Wananchi ”. Alisema Balozi Seif.
Akizungumzia suala la mazoezi Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif alitahadharisha kwamba kitendo cha watumishi wa Sheria kukaa maofisini kwa muda mrefu na baadae kuishia nyumbani bila ya kufanya mazoezi ni hatari kwa afya zao.
Alisema ni vyema kwa watumishi hao kujipangia utaratibu muwafaka wa kufanya mazoezi ya viungo hata kwa siku moja ndani ya wiki ikiwezekana sio mbaya kuyafanyia nyumbani iwapo muda wa kufanya hivyo umekuwa finyu.
Balozi Seif alieleza kwamba mazoezi ni afya kubwa inayomsaidia Jaji, Mwanasheria na Hakimu kufikiri vyema katika utekelezaji wa jukumu lake zito kwa Umma.
Mapema akimkaribisha mgeni rasmi katika falya hiyo Jaji Mkuu wa Zanzibar Mh. Omar Othman Makungu maadhimisho ya Wiki ya Sheria Zanzibar yameamua kuingiza matembezi kwa mara ya kwanza katika ratiba yake ili kutoa fursa
kwa watendaji wa taasisi hiyo.
Jaji Mkuu Makungu alisema miili inahitaji mazoezi na hata matembezi na ilionekana na Uongozi wa Mahakama Kuu kutokana na watendaji waliowengi wanakaa muda mrefu maofisini jambo ambalo ni hatari kwa afya zao.
Alisema changamoto hii ya ukosefu wa kufanya mazoezi kwa baadhi ya watendaji wa Sekta ya Sheria itatoa ushawishi kwao kuanza ukurasa mpya wa kuamua kujiingiza kwenye
eneo hilo muhimu.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/2/2016.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
6/2/2016.