Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua kulia ,Mwl Mkuu Bi Risala na Mjumbe Baraza la UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Amo wakiotesha mti kama ishara uzinduzi wa kilele hicho cha CCM kutimiza miaka 39 .
Katika viwanja vya Arusha Girls High School leo.
Pongezi hizo amezitoa mara baada ya kupokea taarifa za kutoka kwa Mwalimu Mkuu wa Shule hiyo Bi Risala baada ya mjumbe huyo na msafara wake kuwasili shuleni hapo kushiriki upandaji miti ya kivuli na matunda ipatayo 200 kama
sehemu ya maadhimisho ya miaka 39 ya kuzaliwa kwa
Chama Cha Mapinduzi.
Akitoa maelezo hayo Bi Risala alisema kuwa shuleni hapo ,wamekuwa wanajitahidi kuboresha mazingira kwa kuotesha miti pamoja na bustani za mboga kwa ajili ya wanafunzi. Aidha alisema kuwa wanafunzi wanapata taabu ya maeneo ya kupumzikia nyakati za kiangazi kwa kuwa inakuwa ni joto sana, kutokana na ukame katika eneo hilo kwani hapana miti ya vivuli kwa ajili ya kupumzikia wanafunzi nyakati za mapumziko, na kusema kuwa miti hiyo imeletwa kwa wakati muafaka.
Kufuatia taarifa hiyo Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua alitoa pongezi zake na kusema wanachokifanya viongozi hao ni kuunga mkono juhudi za Rais John Pombe Magufuli kupitia kauli mbiu yake yake ya Hapa Kazi Tuu na kuwataka kuendelea kutekeleza kwa vitendo kauli mbiu hiyo, lakini pia akawataka wamuombee Mungu kwa kazi kubwa anayoifanya ya kubana matumizi ,lakini pia ya kutumbua majipu kwa faida ya Watanzania walio wengi ambao ni masikini.
Aidha aliwataka Viongozi wa Shule na wanafunzi hao kuhakikisha wanaitunza miti hiyo , kam sehemu ya kutunza mazingira , lakini pia kwa faida yao kwani matunda hayo yatakuwa ni sehemu ya lishe , lakini kama kumbukumbu kwa wanafunzi wengine watakaojiunga na shule hiyo baadaye.
Pia aliwataka wanafunzi hao kuwa na maadili mema kwa
waalimu , viongozi wao na wazazi ili waweze kufanikiwa
katika maisha yao mbeleni.
Katika maadhimisho hayo mjumbe huyo pamoja na Kiongozi wa Baraza la UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Amo na wanachama aliofuatana nao walishiriki upandaji wa miti kuzunguka
shule hiyo.
Kilele cha maadhimisho ya kuzaliwa CCM Kitaifa kimefanyika leo Februari 6 2016 huko mkoani Singida katika uwanja wa Namfua ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Mwenyekiti wa CCM Taifa Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dk Jakaya Mrisho Kikwete.
Mwisho.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua kulia ,Mwl Mkuu Bi Risala na Mjumbe Baraza la UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Amo wakiotesha mti kama ishara uzinduzi wa kilele hicho cha CCM kutimiza miaka 39,katika viwanja vya Arusha Girls High School leo. .
Mwl Mkuu Bi Risala akiotesha mti katika uzinduzi wa kilele hicho cha CCM kutimiza miaka 39,katika viwanja vya Arusha Girls High School leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua akiotesha mti katika maadhimisho ya kilele cha CCM kutimiza miaka 39 ,katika viwanja vya Arusha Girls High School leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua akichimba shimo la kuotesha mti katika maadhimisho ya kilele cha CCM kutimiza miaka 39 ,katika viwanja vya Arusha Girls High School leo.
Mjumbe Baraza la UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Amo akiwa katika Ofisi ya Mkuu wa Shule ya Arusha Girls High School leo.
Mwalimu Mkuu wa Arusha Girls High School akiwa Ofisini leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua aakiteta jambo na Mwalimu Mkuu wa Arusha Girls High School katika maadhimisho ya kilele cha CCM kutimiza miaka 39 leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua akiwakabidhi miti baadhi ya Wanafunzi , katika maadhimisho ya kilele cha CCM kutimiza miaka 39 ,katika viwanja vya Arusha Girls High School leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua akiwakabidhi miti baadhi ya Wanafunzi , katika maadhimisho ya kilele cha CCM kutimiza miaka 39 ,katika viwanja vya Arusha Girls High School leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua akiwakabidhi miti baadhi ya Wanafunzi , katika maadhimisho ya kilele cha CCM kutimiza miaka 39 ,katika viwanja vya Arusha Girls High School leo.
Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha, Ndg Jasper Kishumbua akiwakabidhi miti baadhi ya Wanafunzi , katika maadhimisho ya kilele cha CCM kutimiza miaka 39 ,katika viwanja vya Arusha Girls High School leo.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua.