Home » » Kairuki awageuzia kibao Tasaf

Kairuki awageuzia kibao Tasaf

Written By CCMdijitali on Sunday, February 14, 2016 | February 14, 2016

Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki.
Kwa ufupi
Pia ameagiza kufanyika ukaguzi maalumu wa fedha za Serikali.
Akizungumza katika Makao Makuu ya Tasaf jijini hapa juzi, Angela alisema anataka ukaguzi wa kina ufanyike kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).



By Vicky Kimaro, Mwananchi vkimaro@mwananchi.co.tz


Dar es Salaam. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Utumishi na Utawala Bora, Angela Kairuki ametoa siku 30 kwa uongozi wa Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (Tasaf) kujitathmini na kutoa ufumbuzi wa haraka ili kuboresha mradi wa awamu ya tatu unaoendelea kwa kaya maskini nchini.

Pia ameagiza kufanyika ukaguzi maalumu wa fedha za Serikali.

Akizungumza katika Makao Makuu ya Tasaf jijini hapa juzi, Angela alisema anataka ukaguzi wa kina ufanyike kupitia Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Katika masuala ya fedha nitakuja sana kukagua zilikuwaje, zimetokaje, kapewa nani, kiasi gani na kama zimemfikia mlengwa,” alisema.

Alisema kwamba haiwezekani kutumia mabilioni ya fedha na ikatokea zikatumika kinyume na malengo kisha taarifa kutolewa vinginevyo.

“Hii siyo sawa ni lazima tuhakiki namna matumizi yalivyo katika ngazi ya kata na watendaji vijijini kama wanatekeleza majukumu yao ipasavyo,” alisema.

Waziri alisema lengo la Serikali ni kuona kila senti ya umma inafanya kazi inayostahili na kwamba, hakutakuwa na msamaha kwa watakaozitumia tofauti.

Awali, Mkurugenzi Mtendaji wa Tasaf, Ladislaus Mwamanga alisema mafanikio ya mradi huo yanakwamisha ukusanyaji wa taarifa kutokana na wakusanya takwimu kutoka katika vijiji vya wanufaika.

Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link