Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu,leo amewasili Jijini Arusha ,tayari kwa Mkutano wa Udhibiti wa Silaha ndogo ndogo katika Kanda ya Afrika,ukikutanisha Washiriki wa Nchi zaidi ya 15.
Mapokezi hayo yameongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Daudi Felix Ntibenda katika uwanja wa ndege wa kimataifa wa Kilimanjaro
Wakazi wengi walionekana kujipanga kando kando ya barabara kuu ya Moshi -Arusha
Baadhi ya Viongozi wa Serekali na Chama Cha Mapinduzi walishiriki katika mapokezi hayo leo katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro
Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu,akishuka kutoka kwenye ndege ,mara baada ya kutua Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Baadhi ya umati wa watu waliojitokeza kumlaki katika Uwanja wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Kama inavyoonekana ,pembezoni mwa barabara kuu ya Moshi -Arusha, baadhi ya watu waliacha shughuli zao ,kumlaki Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu
Baadhi ya Viongozi wa Chama Cha Mapinduzi kutoka nafasi mbalimbali, (kushoto) ni Bi Esther Maleko,Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Mkoa wa Arusha,Mwenyekiti wa CCM Kata ya Unga Ltd - Bi Sophia Munisi,Kada wa CCM Bi Tausi na aliyesimama nyuma yao ni Mwenyekiti wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg Martin Munisi.
Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Arusha NdgSabaya akisalimiana na Mkurugenzi wa Maji Safi na Maji Taka Mkoani Arusha.
Wamama nao hawakuwa nyuma,pichani ni Muasisi wa Chama Cha Mapinduzi ,maarufu kwa jina la Bibi Ndoyee wa Kaloleni,Jijini Arusha.
Kada na Kiongozi wa Chama Cha Mapinduzi na Mfanyabiashara maarufu Jijini Arusha
Alhaji H.Migire
Katibu wa UVCCM Wilaya ya Arusha Ndg jamal Kimji,Katibu Msaidizi wa CCM Wilaya ya Arusha Ndg Elia Ngowi na Rajabu Mshana Kiongozi wa UVCCM Kata ya Sokon I
Katibu Hamasa wa UVCCM Mkoa wa Arusha Ndg Lucas Paschal Nsomi na Mwenyekiti wa Serekali ya Mtaa wa Olmuriaki,Kata ya Sombetini alipita bila kupingwa kwenye uchaguzi mdogo uliofanyika tarehe 17/04/2016, baada ya mgombea wa Chadema ,kuandika barua ya kujitoa,bada ya kuona majimazito.
Mwenyekiti wa UWT Mkoa Bi Zelote na Katibu wake Bi Fatuma Hasan
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Daudi Felix Ntibenda,akiwa tayari kwenda kumpokea mgeni wake.
Bi Viola ,Mjumbe wa Kamati ya Siasa ya Wilaya ya Arusha akiwa na Bi Anna Msuya, tayari kumlaki Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu,kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Daudi Felix Ntibenda,akisalimiana na baadhi ya Viongozi wa dini kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mh Daudi Felix Ntibenda,akimlaki Makamu wa Rais Mama Samia Suluhu kwenye uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Kilimanjaro leo.
Picha zote na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha - Ndg jasper Kishumbua