Home » » Viongozi wa CCM Kata ya Muriet ,wampongeza Mhe. Rais Dk John P. Magufuli

Viongozi wa CCM Kata ya Muriet ,wampongeza Mhe. Rais Dk John P. Magufuli

Written By CCMdijitali on Saturday, May 28, 2016 | May 28, 2016

Viongozi wa CCM Kata ya Muriet ,wampongeza  Mhe. Rais Dk John P. Magufuli kwa kazi kubwa anayoifanya ya kupigania wanyonge walio wengi Tanzania, katika Semina ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata hiyo 28 Mei 2016.

  • Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha awasilisha maelekezo ya Kamati ya Siasa CCM Wilaya,kikao kilichoketi Machi 2016

  • Awataka Viongozi wa Matawi kuwapa heshima na hadhi Viongozi wa CCM wa Mashina na kufanya kazi zote za CCM kwa kupitia kwao kabla ya kuwafikia Wanachama wenyewe.

  • Awasihi Viongozi wake kuwa karibu na wananchi kwa kuwatembelea , kusikiliza kero zao na kuzitafutia majawabu.

Baadhi ya Viongozi wa Mashina Tawi la Terati,  Kata ya Murieti, katika picha ya pamoja mara baada kikao cha Semina ya  Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata hiyo 28 Mei 2016.
 Mwenyekiti wa CCM Kata ya Murieti Ndg Fredy Laizer akimkaribisha katika semina ya Kazi ya Kujenga Chama inayofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha Ndg Jasper Kishumbua aliyekaa  kushoto ni Katibu wa CCM Kata Ndg Saidi Shemdoe.
Katibu wa CCM Kata Ndg Saidi Shemdoe (kulia) akiwa na Mwenyekiti wa WAZAZI Kata Ndg Said Seif Babu ,mara baada kikao cha Semina ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata hiyo 28 Mei 2016.



 Wajumbe wakimsikiliza kwa makini Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha Ndg Jasper Kishumbua alipokuwa anaongea na  viongozi waliofika katika Semina iliyofanyika katika ukumbi wa Ofisi ya CCM Kata ya Murieti 28 Mei 2016.
Ikiwa ni muendelezo wa ziara aliyoianza 18 Aprli 2016 mpaka 05 Juni 2016.

 Ndg Mbaruku Selemani akichangia hoja katika Semina ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata hiyo 28 Mei 2016.



Mwenyekiti wa UWT Bi Mariama Shehondo akiongea na simu mara baada ya Semina ya Kujenga Chama iliyofanywa na Katibu wa Siasa na Uenezi CCM Wilaya Arusha katika Kata hiyo 
28 Mei 2016.

Picha na Idara ya Siasa na Uenezi CCM Wilaya ya Arusha.
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link