Home » » WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI MFUKO WA BIMA YA TAIFA YA AFYA (NHIF)

WAZIRI UMMY MWALIMU AZINDUA BODI YA WAKURUGENZI MFUKO WA BIMA YA TAIFA YA AFYA (NHIF)

Written By CCMdijitali on Sunday, June 12, 2016 | June 12, 2016

Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akikata utepe kwenye vitabu ambavyo ni muongozo wa kazi kwa ajili ya Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), ikiwa ni ishara ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam. Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bw.Bernard Konga.Katika hotuba yake, Waziri Ummy ameutaka Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya kuisaidia wizara ya Afya kwa mafanikio ya wizara hiyo yatatokana na utendaji uliotukuka wa Taasisi mbili ambazo ni NHIF na MSD yaani Bohari ya Madawa kutakuwa na mafanikio makubwa kwa wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto. 
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi vitendea kazi Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mama Anne Makinda , mara baada ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam. katikati ni Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akimkabidhi vitendea kazi Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga kulia ni Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mama Anne Makinda , mara baada ya Uzinduzi wa Bodi hiyo, uliofanyika Juni 11, 2016 kwenye Makao Makuu ya Mfuko huo, Kurasini Jijini Dar es salaam.
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu , Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Konga na Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mama Anne Makinda wakiwa katika picha ya pamoja mara baada ya uzinduzi huo jana
 Mwenyekiti wa Bodi Mpya ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF) Mama Anne Makinda akizungumza mara baada ya uzinduzi huo.
 Baadhi ya wafanyakazi wa mfuko huo wakiwa katika uzinduzi huo.

 Eugine Mikongoti, Mkurugenzi wa Huduma na Uendeshaji wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya ya Jamii Tanzania, NHIF akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu wakati akitembelea na kukagua vitengo mbalimbali vya NHIF katikati ni Mama Anne Makinda Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF.
 Ofisa Mawasiliano wa NHIF, Luhende Singu akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu katikati wakati alipotembelea kituo cha huduma kwa wateja kulia ni Mama Anne Makinda Mwenyekiti wa Bodi ya NHIFM.
 MKurugenzi wa Huduma NHIF Bw Raphael Mwamoto akitoa maelezo kwa Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu, Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mama Anne Makinda, Kaimu Mkurugenzi wa NHIF Bw. Bernald Konga na wajumbe wa bodi wakati alipotembelea kitengo cha kuhifadhi nyaraka
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu na Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF Mama Anne Makinda wakitembelea maeneo mbalimbali mfuko huo.
 Baadhi ya wakuu wa vitengo kutoka mfuko wa bima ya Afya NHIF na Wizara ya Afya wakiwa katika uzinduzi huo.
Baadhi ya wafanyakazi wa NHIF na Waandishi wa habari wakiwa katika zuinduzi huo
 Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
 Mkurugenzi Mkuu wa Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya (NHIF), Bernard Kongaakitoa neno katika uzinduzi huo.
 Rehani Athumani Mkurugenzi wa Masoko na Utafiti NHIF akizungumzana kukaribisha wajumbe wa bodi na wageni mbalimbali waliofika katika uzinduzi wa bodi ya wakurugenzi ya Mfuko wa Taifa wa Bima ya Afya NHIF katika makao makuu ya mfuko huo Kurasini jijini Dar es salaam.
Baadhi ya wafanyakazi wakiwa katika uzinduzi huo
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link