Deogratius Ndejembi
Kwa ufupi
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na John Palingo aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.
By Mwandishi Wetu, mwananchi
Dar es Salaam. Rais John Magufuli amemteua Deogratius Ndejembi kuwa Mkuu wa Wilaya ya Kongwa mkoani Dodoma.
Katibu Mkuu Kiongozi, Balozi John Kijazi amesema Ndejembi anachukua nafasi iliyoachwa na John Palingo aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi katika Mkoa wa Songwe.
Uhamisho wa Palingo kwenda wilaya ya Mbozi, umefanywa baada ya Rais Magufuli kuridhia maombi ya Ally Maswanya aliyeteuliwa kuwa mkuu wa wilaya ya Mbozi, kuomba uteuzi wake utenguliwe kutokana na sababu binafsi.