Kwa ufupi
Kesi hizo zitakuwa zinaendeshwa katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Uhujumu Uchumi na tayari majaji 14 wa wataanza kozi maalumu ya siku tano katika Chuo cha Sheria kilichopo Lushoto, Tanga.
By Kalunde Jamal, Mwananchi kjamal@mwananchi.co.tz
Dar es Salaam. Jaji Mkuu, Mohamed Chande amesema jopo la majaji linatarajiwa kuingia darasani ili kujifunza sheria mpya ya kuendesha kesi za ufisadi.
Kesi hizo zitakuwa zinaendeshwa katika Mahakama Kuu, Kitengo cha Uhujumu Uchumi na tayari majaji 14 wa wataanza kozi maalumu ya siku tano katika Chuo cha Sheria kilichopo Lushoto, Tanga.
Amesema hatua hiyo inakuja baada ya wiki iliyopita, Bunge kupitisha sheria ya uhujumu uchumi ya mwaka 2002 ikiwa na maboresho mbalimbali.
“Maeneo yapo tayari na tumeshapeleka wasajili na watendaji wameanza kufanya kazi, baada ya michakato mingine kukamilika kila kitu kitakuwa sawa na majaji wataanza kazi,” amesema Jaji Chande.