Home » » MAMA SAMIA SULUHU ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI (OCEAN ROAD) JIJINI DAR

MAMA SAMIA SULUHU ATEMBELEA TAASISI YA SARATANI (OCEAN ROAD) JIJINI DAR

Written By CCMdijitali on Friday, July 29, 2016 | July 29, 2016

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan ameahidi kuwa serikali itanunua mashine mbili za kisasa za mionzi kwa ajili ya Taasisi ya Saratani ya Ocean Road ambazo zitasaidia kwa kiasi kikubwa utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaoenda kupata matibabu katika Taasisi hiyo.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Sulu Hassan ametoa ahadi hiyo wakati akizungumza na waandishi wa habari mara baada ya kumaliza ziara fupi ya kutembelea Taasisi ya Saratani ya Ocean Road pamoja na Kumtembelea na kumpa pole Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhani Feruzi ambaye anapatiwa matibabu kwenye Taasisi hiyo jijini Dar es Salaam.

Makamu wa Rais amesisitiza kuwa mkakati uliopo wa serikali unalenga kuhakikisha kuwa hali ya utoaji wa huduma za afya na dawa kote nchini unaimarika maradufu ili wananchi waweze kupata huduma hizo kwenye maeneo yao kwa ubora unatakiwa.

Kuhusu uhaba wa wahudumu wa afya katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan ameuahidi uongozi wa Taasisi hiyo kuwa serikali itahakikisha wahudumu hao wanapatikana katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Baadhi ya wagonjwa na wananchi wamepongeza utoaji wa tiba katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road na wameomba serikali iendelee kuipatia taasisi hiyo vifaa vya kisasa vya kutolea tiba kama hatua ya kuboresha utoaji wa matibabu kwa wagonjwa wanaokwenda kupata matibabu ya saratani. 
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Calist P. Mushi mkazi wa mkoa wa Kilimanjaro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na Katibu wa Kamisheni ya Utalii Zanzibar Saleh Ramadhan Feruzi (katikati) ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road.
 
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Ndugu Said Mohamed mkazi wa Mafia ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Mkazi huyo wa Mafia alimueleza Makamu wa Rais juu ya ugumu wa upatikanaji wa Dawa. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akimjulia hali Bi. Maria Maliseli Boniface wa Kilosa Morogoro ambaye amelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road. 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akizungumza na Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Saratani ya Ocean Road Dk. Diwani Msemo (kulia) wakati wa kutembelea Taasisi hiyo iliyopo jijini Dar es Salaam.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu akizungumza na wananchi waliokuja kuwaona ndugu na jamaa zao ambao wamelazwa katika Taasisi ya Saratani ya Ocean Road, Wananchi hao walimueleza Makamu wa Rais haja ya kuongezwa kwa mashine za mionzi suala ambalo Makamu wa Rais aliwajibu kuwa zitafungwa mashine mpya mbili katika mwaka huu wa fedha 2016-2017 ilikurahisisha matibabu.
Na Michuzi blog
Share this article :
 
Support : #BegaKwaBegaNaMamaSamia | JAK | CCM Arusha
Copyright © 2011. CCM Dijitali - All Rights Reserved
Template Created by Creating Website Published by Jasper K
Proudly powered by Blogger
Link