Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye
Kwa ufupi
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa rai hiyo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa tano wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT), uliofanyika Marangu.
Moshi. Serikali imewataka machifu kukomesha mauaji ya vikongwe na migogoro ya ardhi kati ya wakulima na wafugaji.
Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ametoa rai hiyo katika ufunguzi wa mkutano mkuu wa tano wa Umoja wa Machifu Tanzania (UMT), uliofanyika Marangu.
Amesema ili Taifa ‘lipone’ lazima litumie mila na desturi kupitia kwa machifu.
Chifu wa Wazanaki, Jafeti Edward amesema wanaamini kuwa Serikali ipo pamoja nao ili kuwasaidia watambulike kikatiba kwani shughuli wanazofanya katika jamii zina mchango mkubwa.